Mejja: Niko tayari kufanya collabo na Embarambamba kama ngoma itakuwa vibe

Lakini msanii huyo alisema ikiwa itafanyika, yeye hawezi kushiriki sarakasi za kujigaragaza matopeni.

Muhtasari

• "Siku zote huwa niko wazi na ninasikiliza wimbo wowote ukisikika na kunifanya nijisikie vizuri” Mejja alisema.

Mejja amesema yeye hana shida kufanya collabo na Embarambamba
Mejja amesema yeye hana shida kufanya collabo na Embarambamba
Image: Instagram, fACEBOOK

Msanii Mejja amefunguka kwamba yeye hatakuwa na shinda iwapo msanii mwenye utata mkubwa kutoka Kisii Embarambamba atamfuata na kumtaka kufanya ngoma ya pamoja naye, almaarufu collabo.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee kweney kituo kimoja cha redio humu nchini alasiri ya Ijumaa, Mejja alisema haya hawezi kubagua msanii yeyote kufanay collabo naye bora ana mistari na mihemko ya kufanya ngoma iuze vizuri kwani mwisho wa siku kinachoangaliwa ni mapato kutokana na kazi hiyo ya muziki.

Mejja ila aliweka misimamo yake kwa utani kwamba hata ingawa ataridhia kusshirikishwa au kumshirikisha Embarambamba kweney ngoma, katu hatoweza kushiriki katika sarakasi za msanii huyo amabye anakimbia na kufanya sarakasi za kuhatarisha maisha kabisa.

"Kama ni vibe, kwa nini isiwe hivyo. Lakini siwezi kujikunja kwenye matope na kufanya sarakasi kama zile za kukimbia na kuparamia mitini. Siku zote huwa niko wazi na ninasikiliza wimbo wowote ukisikika na kunifanya nijisikie vizuri” Mejja alisema.

Embarambamba ni msanii aliyekuwa akiimba nyimbo za kudunia kabla ya kudai kwamba amepokea utakaso na kuanza kuimba nyimbo za injili ambazo katika video zake anashiriki visa vya kujiburuza matopeni, kukwea mitini na wakati mwingine kurarua nguo zake hadi kubaki matambara akiwa anatumbuiza.

Ila hilo kwamba Embarambamba ni msanii wa injili halikuonekana kuwa tatizo kwa Mejja kwani alisema yeye huwa anasikiliza midundo kwanza na kama itamvutia bila shaka atajitoa kufanya collabo, bora ngoma ipate mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki.

"Ninapenda kutenganisha mistari yangu kwa sababu sioni sababu ya kufunika nyimbo hizo kwa maneno ikiwa ni za kufurahisha. Naanza na midundo ili niweze kucheza na ala za mpigo. Ninasikiliza midundo ili ninapotunga mistari yangu, midundo yangu ikinibamba, nijue mahali pa kuweka maneno yangu ili kuacha nafasi.” Mejja alieleza.

Mejja ni msanii mkongwe ambaye alikuwa kiongozi wa kundi la The Kansoul kabla ya kundi hilo kuvunjika na kila mmoja kuanza kung’aa kivyake. Umaarufu wake mkubwa kama msanii wa kujitegemea ulikuja mwaka 2020 wakati wa janga la Korona.