Mtoto hana haki ya kuhukumu - Steve Nyerere amshauri Ommy Dimpoz

Nyerere alimtaka Dimpoz kutomhukumu mzee babake kutokana na matukio ya awali sababu hajui kilichotokea baina yake na mamake.

Muhtasari

• “Ushauri wangu kwa Dimpoz ni kwamba kila binadamu ana historia yake. Ukianza kuuliza kwamba kwa nini baba na mama walikosana, huwezi kupata jibu" - Nyerere.

Steve Nyerere amshauri Ommy Dimpoz kutomhukumu babake
Steve Nyerere amshauri Ommy Dimpoz kutomhukumu babake
Image: Instagram

Muigizaji Steve Nyerere amemkunjia msanii Ommy Dimpoz kwamatamshi aliyoyatoa kwenye video yake kuelezea chanzo cha kutokuwa na ukaribu na babake mzee faraji Nyembo.

Nyerere katika mahojiano na wanablogu, alitilia kwenye mizani suala hilo kati na Ommy na babake na kusema kwamba msanii Dimpoz alikosea kwa matamshi yake yale aliyoyatamka dhidi ya babake kwamba kamwe hana mapenzi naye na hawezi kuwa na ukaribu naye.

Ommy Dimpz aliamka maneno yenye ukakasi mkubwa kwenye video hiyo ya uchungu akielezea kwamba mzee wake alitoroka hata hakuhudhuria msiba wa mamake na alimtelekeza moja kwa moja mtoto ambaye sasa ni staa mkubwa mwenye jina lake Ommy Dimpoz.

Alizidi mbele zaidi na kusema kwamba yeye alishaweka kwenye kuchwa chake kwamba mzee wake alikwepa kumlea kwa vile alikuwa ni mtoto haramu na kumtamkia laana kwa Mungu.

Sasa Nyerere anaona si haki kwa Dimpoz kufanya hivyo na amemshauri kukoma kumtelekeza mzee wake kwa vile alimtelekeza awali kwani katika hali ya ustaarabu haifai kabisa mtu kulipa mabaya kwa mabaya.

“Ushauri wangu kwa Dimpoz ni kwamba kila binadamu ana historia yake. Ukianza kuuliza kwamba kwa nini baba na mama walikosana, huwezi kupata jibu. Kila mmoja atasema akijitetea na kwa hiyo wewe utabaki katika nafasi yako kama mtoto. Mtoto hana haki ya kuhukumu,” Nyerere alishauri.

Alisema kwamab kikubwa ni itumike busara na kila kitu kilainishwe nyuma ya kamera na Dimpoz anafaa kujua kwamba mzazi atabaki kuwa mzazi tu siku zote na anahitaji heshima.

Kulingana na Nyerere, huna haki ya kumchukia mzazi mmoja kwa kusikiliza maneno ya mwingine kwani ukianza hivyo utajipata unawachukia wote kila mmoja akikueleza mapungufu na kiini cha kuchukiana na mwingine.