Zari apakia picha za wanawe 5, asema moyo wake umejaa shukrani kwa Mungu

Mioyo yetu imejaa shukrani - Zari

Muhtasari

• Zari alisema kwamba yeye amefanikiwa katika mambo mengi na hana haja ya kulalama bali tu kumshukuru Mungu ndiyo kazi yake kuu.

Zari asema moyo wake umejaa shukrani kwa Mungu kwa kulinda familia yake
Zari asema moyo wake umejaa shukrani kwa Mungu kwa kulinda familia yake
Image: instagram

Mjasiriamali Zari Hassan amepakia picha ya wanawe wote watano kwenye Instagram yake na kumshukuru Mungu kwa kumpa familia maridadi kama hiyo.

Zari ambaye ni mama wa watoto watatu wakubwa kutoka kwa mahusiano yake ya awali na marehemu mumewe, alikuja akaoleka na msanii namba moja wa muda wote katika ukanda wa Afrika Mashariki, Diamond Platnumz na kuzaa na yeye watoto wawili pia.

Zari alisema kwamba yeye amefanikiwa katika mambo mengi na hana haja ya kulalama bali tu kumshukuru Mungu ndiyo kazi yake kuu.

“Baadhi yetu tuliacha kumuomba Mungu vitu vingi sana kwa sababu mioyo yetu imejaa shukrani,” Zari aliandika kwenye picha hizo za kupendeza.

Wengi wanamfagilia sana Zari kwa kile wanasema ana Ngozi mbichi licha ya kuwa na umri mkubwa pamoja na watoto wakubwa sana. Wengine hawaamini kama mfanyibiashara huyo ndiye mama wa vijana watatu wakubwa kwani wengi wanamuona kama ni mama wa watoto hao wadogo waliofanikiwa na Diamond enzi wakiwa pamoja.

Zari pia kwa upande wake ana mapungufu yake kwani baada ya kuachana na Diamond, amekuwa akionekana katika siku za hivi karibuni akitoka kimapenzi na wanaume wadogo kuimri kumliko, jambo ambalo limekuwa likimkosanisha na wafuasi wake mitandaoni, baadhi wakimsuta kwa kujikosea heshima.

Licha ya makali hayo kutoka kwa watu, Zari amebaki kwenye njia yake kuu kwa kutetea hatua yake ya kutoka kimapenzi na vijana wadogo katika kile anakisema kwamba ni chaguo lake na kusema hata wanaume wanaruhusiwa kutoka kimapenzi na wanadada wadogo na hilo halizungumziwi ila mwanamke akitoka kimapenzi na kijana mdogo linakuwa mjadala, kwa nini.