Fahamu wanaume ambao Zari ametoka nao kimapenzi tangu kifo cha mume wake wa kwanza

Zari aliivunja ndoa yake ya miaka 12 na aliyekuwa mumewe wa kwanza marehemu Ivan Ssemwanga.

Muhtasari

• Mfanyibiashara huyo alijizolea umaarufu kutokana na ukaribu wake na msanii Diamond Platnumz mwaka 2014.

Zari Hassan, Diamond Platnumz
Zari Hassan, Diamond Platnumz
Image: Facebook///DiamondPlatnumz

Zari Hassan ni mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa katika maisha yake, ndani na nje ya mitandao ya kijamii. Na kikubwa ambacho kinawavutia wengi ni dhana mbalimbali zinazozunguka maisha yake ya kimapenzi.

Huku wengi wakiwa ni mashabiki zake, lakini ni wachache sana ambao wanajua maisha yake ya kimapenzi. Hapa tunakuandalia orodha ya baadhi ya wamaume ambao mwanamama huyo amekuwa akitoka nao kimapenzi.

Ivan Ssemwanga

Diamond Platnumz

Wengi walimfahamu zaidi Zari kutokana na umaarufu aliojizolea kwa kuwa karibu na msanii Diamond Platnumz. Inasemekana kwamab wawili hao walikutana katika ndege wakati mrembo huyo aliomba kupiga picha na msanii huyo na mwaka 2014 walioana na kubarikiwa na watoto wawili kabla ya mahusiano yao kuvunjika mwaka 2018.

King Bae

Mahusiano ya Zari na mwamba huyu yaliwekwa wazi siku ya Valentino ambapo Zari alipakia picha zake pamoja na zawadi alizozipokea kutoka kwake. Katika picha hizo, Zari alimtambulisha kwa jina King Bae na kummiminia sifa tele kama chaguo rasmi la moyo.

Williams Bugembe

Huyu ni mwanaume ambaye alionekana kuwa na ukaribu sana na Zari wakati wa hafla ya mazishi ya marehemu mumewe wa kwanza Ivan Ssemwanga. Ingawa wengi hawakuweza kujua wazi kama walikuwa katika mahusiano lakini vitendo vyao viliwafanya kusadiki wawili hao huenda walikuwa wapenzi wa kisiri.

Dark Stallion

Zari na Dark Stallion walichukua video pamoja, ambayo iliwekwa kwenye Instagram katika mazingira ambayo ilisemekaan ni mmoja wa meneja wake walitembelea. Ziara hiyo ilikuja siku chache baada ya Zari kuchapisha chapisho lililoashiria kwamba yeye na Dark Stallion walikuwa wameachana. Mashabiki wake wamechanganyikiwa kuhusu iwapo alikuwa ameachana na mume wake au ikiwa ilikuwa ni utangazaji tu.

GK Choppa.

gk choppa na zari
gk choppa na zari

MpakaZari mapema mwaka huu alionekana akiwa pamoja na kijana huyo ambaye wengi walisema ni mdogo kiumri kumliko na kuanza kumpasha.

GK Choppa alionekana akimbusu sosholaiti huyo na kumweka karibu yake huku Zari akionekana kustarehe mikononi mwake. Walakini, watatu hao waliachana miezi mitatu tu baada ya kufahamiana.

Shakib Cham

Huyu dogo ndiye wa hivi punde kuingia kwenye orodha ya kurina asali kutoka kwa mzinga huo usiojua kuzeeka. Pamoja na Zari walianza kuonekana mapema mwezi Juni ambapo mpaka sasa wamekuwa wakionekana pamoja.

Zari hivi juzi amesema kwamba dogo huyo yupo tayari kukutana na wazazi wake na hata kumtolea mahari kama mkewe kabisa.