Mamangu alisema nilizaliwa siku kama leo nikiwa mweusi, kichwa kikubwa - Muigizaji Nyaboke Moraa

Heri njema ya kuzaliwa mama wa wengi - Nyaboke Moraa alijisherehekea.

Muhtasari

• Najipenda sana. Heri njema ya kuzaliwa mama wa wengi, 38 inaonekana nzuri kwako,” alijisifia kwenye picha yake - Moraa alijisherehekea.

Muigizaji Nyaboke ajisherehekea kufikisha miaka 38
Muigizaji Nyaboke ajisherehekea kufikisha miaka 38
Image: Instagram

Muigizaji Nyaboke Moraa leo anasherehekea mika 38 ya kuzaliwa, na kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanamama huyo ambaye anapenda kujiit gaidi ameachia ushauri wa utani kwa wanadada wenzake.

Kulingana na Moraa, mwanamke ukitaka kujua kwamba bwanako au mchumba wako wa kiume anakupenda, inafaa umpe wakati mgumu na hata ikiwezekana umsababishie msongo wa mawazo.

Nyaboke Moraa anawashauri wanadada kwamba ukitaka kujua kama bado mapenzi yake yako kwako, basi hakikisha unampa fikira nyingi, msongo wa mawazo na kila kitu cha kumtatiza akili.

“Wakati mwingine mpitishe huyo mtu wako katika msongo wa mawazo ili kuwa na uhakika kuwa anakupenda,” Moraa aliandika kwenye picha yake ya jana.

Katika picha ya leo, alijisifia na kujisherehekea kwa kufikisha miaka 38 ambapo alijitania kwamba ni mama wa watoto wengi.

“Huyu malkia alizaliwa leo saa tano kamili, akiwa mweusi kabisa na kichwa kubwa kulingana na maneno ya mamangu. Najipenda sana. Heri njema ya kuzaliwa mama wa wengi, 38 inaonekana nzuri kwako,” alijisifia kwenye picha yake.

Nyaboke alikuwa ameolewa na staa wa mchezo wa ruji humu nchini marehemu Benjamin Ayimba ambaye mpaka kifo chake mwaka jana Mei, alikuwa ashaichezea Kenya 7s pamoja pia na kuwa kocha wao.

Nyaboke walikuwa wametengana na Ayimba hata hivo lakini kifo chake kilimuumiza sana ambapo alimuomboleza kipindi hicho kwa kujiuliza maswali kwamba ni nini atawaambia watoto wake watakapomuuliza baba yao yuko wapi.