King Kaka apakia picha ya pamoja na wanawe, asema anajifunza kuwa baba bora

Katika picha hiyo, aisema yumo mafunzoni kuwa bora kwa wanawe

Muhtasari

• Msanii King Kaka kwa mara ya kwanza katika muda mrefu amepakia picha ya pamoja na wanawe na kupata sifa tele kuwa baba bora.

King Kaka apakia picha na wanawe
King Kaka apakia picha na wanawe
Image: Instagram

Mwanamuzimi na mjasiriamali Kennedy Ombina almaarufu King Kaka amechokoza mtandao wa Instagram kwa kupakia picha ya wanawe wawili, picha ambayo wengi wameifagilia sana.

Katika picha hiyo, King Kaka alidokeza kwamba ako katika mafunzo ya jinsi ya kuwa baba, na kusema anajifunza kutoka kwa wanao hao jinsi ya kuwalea kama baba mzuri.

“Masomo ya kuwa baba, najifunza kutoka kwa hawa wawili Prince Iroma na Royal,” King Kaka aliandika.

Wengi katika mitandao ya kijamii wamemmiminia sifa kocho kocho msanii huyo kwa kujitahidi kuwaonesha watoto wake mapenzi.

Wengine walitolea mfano kwamba katika dunia ya sasa ambapo idadi ya watoto wasiokuwa na baba inazidi kuongezeka, ni nadra sana kwa mtu kupata amepewa shavu na babake.

Wengine walisema kitu cha muhimu kabisa unaweza ukampa mtoto katika umri wake mdogo ni mapenzi ya baba na kuwataja watoto hao kama wachache miongoni mwa kundi kubwa la watoto wanaolilia ngoa kuwa karibu na baba zao kama hao.

Hilo pia liliibua mafunzo kadhaa kutoka kwa wasanii Miracle Baby na Ommy Dimpoz ambao wamejitokeza wazi na kuwakana wazee waliodai kuwa baba zao wa kuwazaa.

Kwa upande wa Ommy, alisema kwamba hana mapenzi na babake kwa vile hakuwahi kuwa na ukaribu naye na hawezi kuwa na ukaribu naye. Pia alisema mzee huyo alimnyima mapenzi ya baba kwa mtoto kipindi cha utoto wake.

Kutokana na matukio hayo yanayoendelea Sakata kati ya baba na watoto, wengi wamemsifia King Kaka kwa kusimama na wanawe na kuchukua picha kama hiyo ni swehemu moja ya kuweka kumbukizi nzuri za siku zijazo.