Vera Sidika aadhimisha miaka 10 kama mwanasosholaiti

Licha ya Vera kutokuwa mitandaoni sana amekuwa akivuma mitandaoni kwa mambo kadha wa kadha.

Muhtasari
  • Upande wake wa nyuma ulipata kuzingatiwa na tangu wakati huo ameorodheshwa miongoni mwa wanasosholaiti wenye ushawishi mkubwa nchini Kenya

Mwanasoshoaliti maarufu nchini Vera  Sidika siku ya leo anaadhimisha mika kumi kama mwanasosholaiti.

Licha ya Vera kutokuwa mitandaoni sana amekuwa akivuma mitandaoni kwa mambo kadha wa kadha.

Vera kupitia kwenye ukurasa wake wa insaram amesema kwamba kwa miaka yake 10 kama mwanasosholaiti amekuwa akizungumziwa sana.

Vera amebarikiwa na mtoto mmoja pampja na mpenzi wake msanii Brown Mauzo.

Katika dokezo kuhusu kuwa maarufu kwa muda huo Vera aliandika

"Desemba 17, 2012, hii ndiyo tarehe niliyopata umaarufu kwa video ya muziki iliyozua utata. Tarehe 17 Desemba 2022 mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 10!!! wow.."

Bi Mauzo aliongeza;

"Nimekuwa maarufu kwa miaka kumi nzuri. Fikiria na bado kuwa juu ya mchezo wangu. Hata ninapokaa kimya kwa miezi au miaka bado nina-trend na kwa namna fulani kupata watu kuzungumza hata nisipokuwepo."

Kwa wale ambao hawajui, alionekana kwenye video ya "You guy" ya P Unit.

Upande wake wa nyuma ulipata kuzingatiwa na tangu wakati huo ameorodheshwa miongoni mwa wanasosholaiti wenye ushawishi mkubwa nchini Kenya.