Video ya DP Gachagua akicheza densi ya Mugithi na mkewe yafurahisha wanamitandao

Gachagua aliipakia video hiyo kwenye Facebook yake kipindi bado kampeni zikiendelea

Muhtasari

• Video hii yenye Kumbukumbu hiyo tamu inajiri wakati naibu rais akiongoza nchi kufuatia ziara ya rais William Ruto ughaibuni.

Mitandao ya kijamii Imejawa na bashasha baada ya video ikimuonesha naibu rais Rigathi Gachagua akicheza densi na mkewe kuibuka.

Video hiyo inayodhaniwa kuchukuliwa nyumbani kwake muda fulani nyuma akiwa mbunge wa Mathira inamuonesha Gachagua akicheza densi kwa mbwembwe na mwendo wa taratibu nyimbo ya Kikuyu almaarufu Mugithi.

Naibu rais amekuwa akizungumziwa katika mitandao ya kijamii kwa dhana mbali mbali kutoka kwa mavazi yake hadi uongeaji wake, ila video hii kwa mara ya kwanza imewafanya Wakenya kumzungumzia kwa njia chanya.

Wengi walimsifia kwa kusema kwamba amevunjilia mbana dhana ya kuonesha wanaume wanasiasa hawana muda wa kuonesha mahaba kwa wachumba wao kutokana na mishe nyingi za hapa na pale.

Video hii yenye Kumbukumbu hiyo tamu inajiri wakati naibu rais akiongoza nchi kufuatia ziara ya rais William Ruto ughaibuni.

Ruto aliondoka nchini mapema wiki hii kuelekea nchini Uingereza kuhudhuria msiba wa aliyekuwa malkia wa muda mrefu Elizabeth wa pili na baadae akatimba kwenye pipa kuelekea Marekani kuhudhuria kongamano la 77 la umoja wa mataifa.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii walifurahishwa na hatua zilizopangwa kitaratibu za uchezaji densi wa naibu rais Rigathi Gachagua na mkewe na kuongeza kuwa Gachagua kwa mara ya kwanza amedhihirisha upande wa maisha yake ya kimahaba, kinyume na minong’ono ya wengi.

Wengine walimsifia kwa kumpenda na kumuonesha mkewe mchungaji Dorcas Gachagua mapenzi hadharani.

Ikumbukwe siku ya kuapishwa kama naibu rais, Gachagua alitoa kauli moja iliyowafurahisha wanandoa wengi aliposema kwamba hata uwe nani, unafaa kuheshimu sana familia yako kwa vile ndio watu pekee wa karibu wanaoweza kukupa shavu wakati mambo yako yatakwama.