Mtu wa kwanza kumpa kadi ya mwaliko katika harusi yangu ni Ex wangu - Ruby

Ruby alisema kwamab hatotoa kadi hiyo kwa sababu ya bifu bali tu kwa kumtaka kufika kuona jinsi anavyovishwa pete.

Muhtasari

• Niseme tu kwamba, katika kadi ambazo nitazisambaza za Mualiko kwa watu kuja kwenye Harusi yangu - Ruby.

msanii Ruby asema atampa kadi ya harusi yake Ex wake.
msanii Ruby asema atampa kadi ya harusi yake Ex wake.
Image: instagram

Msanii wa bongo fleva Ruby amefunguka kwamba yeye wala hana uhasama wowote na mpenzi wake wa awali.

Ruby akizungumza na kituo cha redio cha EFM katika kipindi cha Uhondo, alisema kwamba ikatokea harusi yake, mtu wa kwanza kumpa kadi ya harusi atakuwa mpenzi wake wa zamani, yaani Ex.

“Ikitokea sasa baba mtoto wako ndio arusi anakuoa, Ex wako unaweza ukampa kadi ya harusi akaja kuhudhuria?” mtangazaji alimuuliza swali la chokoza.

“Huyo ndio atakuwa wa kwanza. Niseme tu kwamba, katika kadi ambazo nitazisambaza za Mualiko kwa watu kuja kwenye Harusi yangu, Ex wangu atakuwa mtu wa kwanza kuipata ili aje tu ashuhudie wala si kwamba nitampa mwaliko kwa bifu au nini, ni kumualika tu aje kushuhudia ninavyoolewa,” Ruby alizungumza.

Msanii huyo pia aliulizwa kuhusu kunyamaziana kwake na mwigizaji mkongwe Aunty Ezekiel ambapo alisema kwamba hawajawahi zungumza na wala hawana ugomvi baina yao.

Ruby aliweka wazi siku kadhaa zilizopita kwamba ana mpenzi na wanapendana sana ila akadinda kabisa kumtambulisha kwenye mitandao ya kijamii.

Alisema kwamba mpenzi huyo ni mtu wa kawaida wala si msanii kabisa, na kusema ikifika muda watu watamuona.

“Yeye ni mtu tu wa kawaida, ana biashara yake na kazi yake ni tofauti kabisa na yangu,” Ruby alisema.

Katika mazungumzo yote, mwanamuziki huyo alionekana kumzungumzia kwa njia hasi sana baba mtoto wake na hata kukataa kabisa uwezekano wa kuweka mambo sawa kwa ajili ya mtoto siku za mbeleni.