Picha ya Amber Ray na aliyekuwa mpenzi wa Betty Kyallo, Nick Ndeda yataniwa mitandaoni

Nick Ndeda waliachana na Betty Kyallo miezi kadhaa iliyopita huku Amber Ray akiachana na Rapuda wiki chache nyuma.

Muhtasari

• Itakumbukwa kuwa maisha ya kimapenzi ya wawili hao haijakuwa moja ya kutumiwa kama mfano mzuri wa watu waliofurahikia mapenzi.

Amber Ray na Nick Ndedqa kweney picha moja
Amber Ray na Nick Ndedqa kweney picha moja
Image: Instagram

Mwanamitindo Amber Ray Alhamis alipakia picha ya pamoja na wakili Nick Ndeda, aliyekuwa mpenzi wa mwanahabari wa runinga wa muda mrefu, Betty Kyallo.

Wawili hao walionekana kwenye picha nzuri na tabasamu zilizohanikiza kote kote huku Ray akidokeza kwamba katika maisha yake ameamua kuchagua ukarimu kwa sababu anajua jinsi ni vigumu kwa ukarimu huo kuja.

“Ninachagua fadhili kwa sababu najua jinsi ilivyo ngumu kupata. Ninachagua watu wanaoinuka kutoka kuzimu kwa tabasamu kwa sababu polarity yao inatia moyo,” Amber Ray aliandika huku akimtag mwanasheria Nick Ndeda ambaye pia alidhibitisha kwa kusema hilo nalo ni neno kwa kweli.

Picha ya wawili hao ilizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi wakitania kwamba hivi karibuni huenda watazidi kuwaona pamoja kama marafiki wa karibu mno.

Itakumbukwa kuwa maisha ya kimapenzi ya wawili hao haijakuwa moja ya kutumiwa kama mfano mzuri wa watu waliofurahikia mapenzi.

Nick Ndeda miezi michache nyuma aligonga vichwa vya habari baada ya kuweka wazi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanahabari Betty Kyallo na baadae wakatengana kwa ukimya na usiri mkubwa. Hakuna aliyejitokeza kuweka wazi kisa au sababu ya kuvunja mahusiano yao.

Kwa upande wake mwanamitindo Amber Ray, pia amekuwa na panda shuka katika mahusiano yake ambapo mapema mwaka huu aliachana na mfanyibiashara Jimal Rohosafi na mpaka kuifuta tattoo yake mgongoni.

Kisha baadae alikuja akaingia kwenye mahusiano na mchezaji wa mpira wa vikapu kutoka Sierra Leone Ib Kabaa amabye hawakudumu kwa muda mrefu kabla tena ya Ray kuibua mwamba kwa jina Kennedy Rapudo ambaye hivi majuzi wamedokeza kuwa hawako pamoja tena.