Tiktoker Azziad azuru South Africa, apakia picha akijivinjari mitaani humo

Azziad alijizolea umaarufu kwenye Tiktok mnamo mwaka 2020 kwa kibao cha Utawezana.

Muhtasari

• Wiki chache zilizopita Azziad alichangamsha Tiktok kwa klipu ya wimbo wa vaida ambacho kiliwavutia wengi mpaka seneta wa Kakamega.

Azziad Nasenya akila bata Afrika Kusini
Azziad Nasenya akila bata Afrika Kusini
Image: Instagram

Malkia wa TikTok nchini Kenya, Azziad Nasenya ambaye pia anajiongeza kama mtangazaji wa rdio ya Sound City amepakiwa picha maridadi akiwa anakula bata nono katika jamhuri ya Afrika Kusini.

“Afrika Kusini kuna yepi mazuri?” Azziad aliandika kwenye Instagram yake.

Azziad alijizolea umaarufu kwenye Tiktok mnamo mwaka 2020 wakati shughuli nyingi kote ulimwenguni zilikuwa zimesitishwa na maeneo mengi kusalia mahame ambapo wengi walikuwa wanajiburudisha na klipu za mtandao huo mpya kabisa nchini kipindi hicho.

Baada ya kuonekana akifanya klipu cha wimbo maarufu wakati huo, collabo iliyowakutanisha magwiji Mejja na mwanamuziki wa kike mkali katika kuchana mistari, Femi One kwa jina Utawezana, nyota ya Azziad iling’aa ghafla.

Wengi walimsifia kwa unenguaji wake kwa kibao hicho na hapo ndipo brand yake ilikua na kuvutia biashara nyingi kumfuata kutaka kutangaza biashara zao katika ukurasa wake wa TikTok na wengine kumpa mkataba wenye posho la kishua kuwa balozi wao wa mauzo.

Baadae alipata kazi kwenye kituo cha redio cha Sound City jijini Nairobi na amezidi kuwafurahisha wengi TikTok, kitu ambacho kimemfanya kuzuru mataifa mbali mbali kama mtalii kujifurahisha.

Baada ya kimya cha muda, Azziad wiki chache zilizopita alikuja kwa vishindo ambapo alifanya kile anachokifanya kwa umahiri mkubwa – klipu ya ngoma na safari hii alirudi nyumbani na kujaribu wimbo wa Vaida.

Klipu hiyo chini ya siku moja kilipata watazamaji zaidi ya milioni moja ambapo mpaka seneta wa Kakamega Boni Khalwale alifurahishwa nacho na kukinukuu kweney ukurasa wake wa Twitter.