Jovial awasuta wanaomuonya dhidi ya kuwa mpenzi wa Willy Paul

Watu wengine wanataka wakuendesha na kukwambia cha kufanya wakati maisha ni yako - Jovial.

Muhtasari

• Jovial alimsuta jamaa mmoja aliyejaribu kumshauri kufuata mkondo wa muziki wake na kuachana na Pozze kwamba atamtumika.

Willy Paul na Jovial wadokeza kuwa kwenye mapenzi
Willy Paul na Jovial wadokeza kuwa kwenye mapenzi
Image: Instagram

Wiki kadhaa zilizopita msanii Willy Paul alirukwa na vichwa mitandaoni na kuanza kuachia jumbe za mapenzi akionekana kumtongoza msanii mwenzake Jovial.

Wengi walisema kwamab huenda kuna collabo mpya iliyokuwa inapikwa na wawili hao na ni kiki tu ya ufuasi walikuwa wanakimbiza katika mitandao ya kijamii mbele ya wimbo wao.

@jovial_ke angalau kuwa na utu. Sikatai watu wanasema mimi ni bwana mkunaji, sijui ni kwa nini.. in life lazima kila mtu anachoka na anaamua kutulia mimi hapa naomba nitulie na wewe.,” Willy Paul Aliandika.

Lakini sasa imechukua mkondo tofauti kabisa baada ya msanii Jovial mwenyewe kupeleka kwenye instastires zake na kuweka wazi kwamba huenda wako katika mahaba mazito na Willy Paul, bosi wa lebo ya Saldido.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jovial alipakia picha ya Willy Paul na kuifuatisha kwa maneno kwamba anahisi kabisa ametumbukia katika shimo la mapenzi ya Willy Paul.

Jovial alionekana kukubaliana na wengi waliochukua ujumbe huo na kuusambaza ambapo naye aliupakia na kuwashukuru kwa kumtakia mema katika safari ya kimapenzi na Willy Paul.

“Mimi nishatumbukia kwenye mapenzi,” Jovial alidokeza huku akifuatisha na picha ya Pozee.

Baadhi walijaribu kumshauri kuachana na mapenzi na kufuata ndoto yake ya muziki, jambo ambalo alionekana kutolifurahia kabisa na kulisuta kwa ujumbe:

“Kuna watu kwenye haya maisha huwa wanataka wakuendeshe na kukwambia cha kufanya na wakati maisha ni yako,” Jovial aliandika kwenye Instastories.

Huku Sakata hili likiendelea kuzungumziwa, baadhi bado wanahisi huenda wawili hao ni collabo wanaendelea kuweka tayari kuitoa na wengine wanasema ndio wapenzi wapya kabisa mjini, ila yote tisa kumi ni kukaa mkao wa kula na kusubiri jinsi matukio yatakapojiri siku za kesho.