•Felicity aliweka wazi kuwa Pluto alikuwa akimpa vidokezo vya kutaka kumzawadi gari ila hakutarajia kabisa kuwa itawahi kufanyika.
MwanaYouTube Felicity Shiru amejibu madai ya baadhi ya wanamitandao kuhusu gari alilozawadiwa na mpenzi wake Robert Ndegwa alimaarufu Thee Pluto.
Felicity alizawadiwa gari hilo bila kutarajia katika hafla ya kumpongeza kwa kuwa kupata ujauzito. Alisema kwamba hakutarajia kuzawadiwa gari siku hiyo na hangeweza kuitisha stakabadhi za usajili wa gari hilo ila tu kumshukuru Pluto kwa zawadi hiyo.
“Sasa ningeanza kumwambia Pluto anipe logbook ya gari? Eti ndio niamini gari ni langu? Sasa karatasi zilikuwa ziendewe wapi?”alisema.
Aliwashauri watu kujifunza kushukuru wanachopewa kitu au kuzawadiwa na kutobagua zawadi wanazotaka kupewa na baadaye akamshukuru mpenzi wake kwa hafla.
“Asante sana Pluto kwa kupanga yote haya kwa ajili yangu, hakuna kitu nimefanya ama kuchangia. Kila kitu kilikuwa shwari ikiwemo chakula, MC na hata burudani. Na pia kwa zawadi uliyonipa leo,sikuwa nimetarajia,”alisema.
Felicity aliweka wazi kuwa Pluto alikuwa akimpa vidokezo vya kutaka kumzawadi gari ila hakutarajia kabisa kuwa itawahi kufanyika.
Wawili hao walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wa kike ingawa Felicity alikuwa akitarajia mtoto wa kiume baada ya kuambiwa na kupata maoni ya watu akiwemo mama yake kuwa uja uzito wake ni wa kiume.