Ukioa karibuni njoo uniite umbwa - Manara amsuta Diamond kwa kusema hivi karibuni anaoa

Diamond aliachia maoni kwenye post ya manara akisema kuwa hivi karibuni ataoa.

Muhtasari

• “Nami niko njiani Inshallah,” Msanii Diamond Platnumz aliandika kwenye picha hiyo ya mkewe Hajji Manara.

Hajji Manara asema Diamond hawezi oa
Hajji Manara asema Diamond hawezi oa
Image: Instagram

Mchambuzi wa masuala ya spoti nchini Tanzania, Hajji Manara Sunday amempiga msanii Diamond Platnumz kumbo la mwaka kwenye mtandao wa Instagram baada ya kumwambia moja kwa moja kwamba hawezi oa kamwe.

Hajji Manara alipakia picha ya mke wake mpya baada ya fununu kuzagaa wiki jana kuwa ametengana na aliyekuwa mke wake.

Alimtambulisha kwa watumizi wa Instagram na kusema kuwa ndiye mke wake mpya na hapo ndipo msanii Diamond Platnumz alifika pale na kuachia maoni kwamba hata yeye yuko njiani kuingia katika ndoa hivi karibuni.

Manara alimrushia utani wa mwaka Diamond Platnumz na kumwambia kwamba hawezi kuoa na kama itatokea ameoa basi amuite Manara umbwa kubwa.

Kwa sasa Mke wangu anafahamika kama @ Ruush Bugati,” Manara aliandika.

“Nami niko njiani Inshallah,” Msanii Diamond Platnumz aliandika kwenye picha hiyo ya mkewe Hajji Manara.

“Ukioa karibuni njoo Rotan unite jibwa,” Manara alimjibu Diamond.

Wengi walizua utani kuwa Manara alikuwa ana maana nyingine kando na hiyo ya kumwambia Diamond kuwa hawezi oa. Walisema kuwa mchanganuzi huyo wa spoti alikuwa anatupa dongo kwa msanii Zuchu kuwa hawezi olewa na Diamond na kama hilo litakuja kutokea basi watu wamwite umbwa tena kwa hali ya ukubwa – jibwa.

Diamond na Zuchu wamekuwa wakisemekana kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna hata mmoja kati yao amewahi kuweka wazi na kudhibitisha wala kupinga minong’ono hiyo.