Willy Paul atangaza kupata mchumba, Jovial, aonya wapenzi wa kitambo

Mwanamuziki huyo alisema kuwa hajali wanachoongea watu kwani yeye na mpenzi wake Jovial wanapendana kwa dhati.

Muhtasari

• Mwanamuziki huyo alisema kuwa hajali wanachoongea watu kwani yeye na mpenzi wake Jovial wanapendana kwa dhati.

 

Willy Paul na Jovial
Image: Wily Paul Instagram

Mwanamuziki Wilson Abubakar Radido almaarufu Willy Paul ayaongelea mahusiano yake na mwanamuziki anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa sasa Juliet Miriam Ayub almaarufu Jovial.

Willy Paul alisema yeye na Jovial wamekuwa familia tayari na kuwa uhusiano wao hauwezi ukavunjwa.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa hajali wanachoongea watu kwani yeye na mpenzi wake Jovial wanapendana kwa dhati.

"Hakuna kitu ambacho kitabadilika hata mkiongea,tushapendana na ni hivyo. Hii picha ya kifamilia iko aje?"alisema.

Aliwaonya na kuwakanya wanadada aliokuwa akiongea nao hapo awali kabla aanze uhusiano wake na Jovial akiwambia kuwa hayo ni mambo yaliyotendeka kabla ya kumpata Jovial.

Willy Paul aliwaambia wapambe kuwa hakuna kitu wataweza kufanya ili kumtenganisha na Jovial ikiwemo kufunga na kwenda kwenye maombi.

"Na kwa wale wasichana pengine tulikuwa na mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea, poleni sana nishapenda kwengine,"alisema.

Msanii huyo aliongeza kuwa Kenya ndio mahali pekee ambapo mtu akipenda ama kuwa kwenye mahusiano linakuwa jambo kubwa .

Haya yaliweza kutendeka baada ya Willy Paul kusemekana kuwa na mazoea ya kumtumia ujumbe mwanadada ambaye ni mpenzi wa wenyewe.

Willy Paul aliwafokea watu baada ya suala hilo kuenea mtandaoni na kusema kuwa yeye na Jovial ni kitu kimoja na hawawezi wakatenganishwa na jambo lolote lile.

"Haha kwani mimi kuwa kwenye uhusiano imeumaje watu. Endeleeni, mimi nishapata wangu," alisema.

Jovial pia aliweka wazi picha yake na Willy Paul mtandaoni na kusema kuwa bado wataendelea kuwa kwenye mahusiano hata watu waseme nini.

"Bado tupo sana, kiwiliwili changu,"alisema.

Hata baada ya mahaba haya yote wawili hawa wameonyesha mitandaoni mashabiki wao wengine bado wanashuku mahusiano hayo na kusema kuwa ni kiki ya wimbo mpya ambao Willy Paul na Jovial wanatafuta.