Baada ya muda mrefu wa kutoonana jicho kwa jicho kati ya wasanii Chipukeezy na Kartelo, hatimaye wachekeshaji hao wawili tena wametangaza kurudi na kufanya kazi pamoja.
Wawili hao walikuwa marafiki wa kufa kuzikana tangu miaka ya nyuma mbapo walikuwa na shoo ya ucheshi ambayo ilikuwa inapeperushwa katika vituo vya runinga za Ebru na TV47 ila baada ya janga la Korona mwaka 2021 walisemekana kukosana vibaya hata kutopigiana simu wala kushabikiana kwenye mitandao ya kijamii.
Kuzungumza vizuri juu ya madai yao ya kutoelewana - wacheshi hao wawili walidumisha urafiki wao bado unaendelea na kwa sababu tu hawaonekani pamoja kwenye mitandao ya kijamii haimaanishi kuwa hawaonani faragha.
Itakumbukwa mchekeshaji Kartelo mapema mwaka huu mwanablogu Mungai Eve alipomtembelea katika moja ya biashara zake huko Kayole, alisisitiza kwamba hakuna kilichoharibika baina yake na Chipukeezy na kuwa urafiki wao ungalipo.
Mungai alimuuliza hilo baada ya Chipikeezy kurejea kutoka marekani na Kartelo ambaye alikuwa rafiki wake wa muda mrefu hakutokeza kwenye angatua ya JKIA kumlaki.
“Sidhani nili-unfollow Kartelo. Sisi ni watu wa mitaa ya mabanda na tuko tu sawa. Hata wewe kwa Instagram yako unaweza pata ume-unfollow, kwa hiyo wacheni kufuatilia mambo duni kama hayo. Kwani tunachumbiani ndio sisi tukiacha kushabikiana kwenye mitandao kila mtu anasema kuna noma?” Kartelo alijibu.
Lakini unaamnbiwa siku zote hakuna uadui wa milele kati ya wanaume wawili waliokomaa na ambao wana akili timamu zilizoboreshwa kwa elimu ya shuleni na duniani. Msanii Chipukeezy kupitia Instagram yake Jumatatu alasiri alidokeza kurudi kwa shoo hiyo yake na kumtaja Kartelo kama mmoja wa watu watakaoianzisha upya kama ilivyo kuwa awali.
“Kurudi kwa shoo ya Chipukeezy, uko tayari Kartelo?” Chipuukeezy aliandika.
Vile vile, Kartelo ambaye mara nyingi hupenda kutumia lugha ya mitaani almaarufu Sheng alipakia picha yao ya pamoja enzi za nyuma na kusema shoo hiyo inasubiriwa sana kwenye runinga.
“Kwa Mbulu mara inengi Chipukeezy (kwa runinga mara nyingine tena Chipukeezy)” aliandika Kartelo.