logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Katibu wa kanisa ajiua kisa mzozo wa kimapenzi na mke wa mchungaji Masanja Mkandamizaji

Katibu wa kanisa la Masanja alijiua kutokana na kile kilitajwa kuwa ni mzozo wa kimapenzi baina yake na mke wa Mchungaji huyo.

image
na Davis Ojiambo

Burudani03 October 2022 - 06:53

Muhtasari


  • • Katibu wa kanisa la Masanja alijiua kutokana na kile kilitajwa kuwa ni mzozo wa kimapenzi baina yake na mke wa Mchungaji huyo.
  • • Masanja alimwandikia mke wake ujumbe kuwa atasimama na yeye mpaka pumzi yake ya mwisho na hatomuacha hata baada ya sakata hilo kutokea.
Mchungaji Masanja Mkandamizaji na mkewe

Wikendi iliyopita kulikuwepo na uvumi wa sakata la kujitoa uhai kwa katibu katika kanisa la Feel Free la aliyekuwa mchekeshaji na mchungaji Masanja Mkandamizaji kutoka Tanzania.

Taarifa zilisema kuwa katibu huyo alijitoa uhai kutokana na kujulikana kwa skendo ya kutoka kimapenzi na mama wa kanisa ambaye ni mkewe mchungaji Masanja Mkandamizaji.

Ujumbemrefu uliovujishwa kutoka kwa marehemu aliuachana kabla ya kifo chake unaelezea kwa mapana sababu za kujitoa uhai katika sakata ambalo sasa limejumuisha mambo mengi likiwemo suala la kuchepuka na mama kanisa.

Barua hiyo alionekana kumwandikia mwanamke mmoja ambaye  bado haijabainika kama kweli ni mkewe Masanja.

“Asante Kwa kunipenda Kipindi chote hakika umenipa Upendo ambao umeacha alama moyoni mwangu ambao kila nikijaribu kuifuta nimeshindwa sioni upendo wako wa Mwanzo hivyo nimebaki Kuumia MOYONI kwa kukosa,” sehemu ya barua hiyo ilisoma.

Mchekeshaji Mkandamizaji ambaye kila Jumapili huwa anahubiri katika kituo cha Wasafi, hakuhudhuria kipindi hicho kutokana na suala hilo tata ambalo linazidi kuchemka haswa kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Masanja Mkandamizaji alipakia video yenye picha ya pamoja na mkewe wakionekana katika mkao wa kuomba na kusujudu vile na kuachia ujumbe changamano ambao wengi waliuambatanisha na sakata hilo la kujitoa uhai kwa katibu katika kanisa lake.

Baada ya watu zaidi ya laki mbili ufurika pale na kuachia maoni mbali mbali, mchungaji Mkandamizaji aliifuta post ile lakini kuna baadhi ya wale waliobahatika kuinakili na ilikuwa na maneno;

“Kila kazi ina gharama yake. Acha tulipe gharama ya tulichoitiwa. Nakupenda mpaka pumzi yangu ya mwisho mke wangu. Hili nalo litapita. Tuombeeni nasi tunaomba. Mtetezi wetu yu hai,” Mkandamizaji aliandika.

Katika maneno haya, wengi walionekana kukisia kuwa mchungaji huyo alikuwa anatia roho ya kiume kusimama na mke wake wakati wa kipindi hiki kigumu ambacho kimezua timbwiri la kumsaliti mume wake na mfanyikazi wa kanisa lao.

Wengine walisema kuwa huenda katibu huyo alijiua si tu kutokana na mzozo wa kimapenzi bali pia kutokana na msongo wa akili na unyongovu.

Sasa basi ikiwa wewe unapitia hali kama hiyo ya mawazo kutatizana kufuatia mambo mbali mbali, Washauri, madaktari na wanasaikolojia wanashauri kwamba unaweza kufikia usaidizi wakati wowote unapokumbana na matatizo yoyote ya afya ya akili. Piga simu ya Kenya Red Cross bila malipo, 1199 kwa usaidizi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved