Zuchu apakia video ya Diamond akifanya sala, asema ndio atakayomkumbuka nayo kila siku

Zuchu alisema video hiyo Diamond akifanya sala ndio njia ya kipekee ya kumkumbuka nayo kila siku

Muhtasari

• Diamond alikuwa anasherekehea siku yake ya kuzaliwa wikendi.

Zuchu aonesha upande wa pili wa Diamond kuwa mchamungu
Zuchu aonesha upande wa pili wa Diamond kuwa mchamungu
Image: instagram

Wikendi ilikuwa siku kubwa sana kwa familia ya mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Wasafi, Diamond Platnumz kwani iliwiana na siku yake ya kuzaliwa pamoja pia na mwanawe Naseej Junior.

Kwa miaka mitatu sasa, Diamond hajawahi jisherehekea katika siku hiyo bali yeye hutumia siku hiyo kumsherehekea mwanawe Naseeb Junior ambaye walipata na mwanamuziki kutoka Kenya, Tanasha Donna, na wikendi hii haikuwa tofauti.

Diamond alipakia picha ya mwanawe na kumtakia kila la kheri huku akifikisha miaka mitatu, ila yeye mwenyewe hakujitamkia kitu chochote na badala yake mashabiki zake wengi walimsherehekea kwa jumbe zenye uhai tele.

Moja ya watu ambao waliachia ujumbe maalumu kwake ni mwanamuziki chini ya lebo yake, Zuchu.

Ujumbe wa Zuchu ulipokelewa kwa njia tofauti na watumizi wa mitandao ya kijamii haswa kutokana na dhana ambayo imekuwa ikisambazwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kuhusu uwezekano wa mahusiano ya kimapenzi baina yake na Diamond.

Kupitia Instagram yake, Zuchu aliwakosha wengi baada ya kupakia picha pamoja na video ya Diamond huku akiambatanisha kwa maneno kuwa, “hivi ndivyo nitakavyokukumbuka kila siku.”

Video ile ilikuwa na maudhui maalumu kwa msanii huyo kwani alionekana akifanya kitu ambacho ni nadra sana kuonekana kutoka kwake.

Diamond alionekana amevalia kama mtoto wa Kiislamu akifanya sala akiwa amesimama na pia mwendelezo wake msanii huyo anaonekana ameketi kitako huku akimega sala za lakka ambazo ni maalumu kwa waumini wa Kiislamu.

Wasanii wengine walijumuika pale na kusema kwamba msanii Zuchu amewaonyesha upande wa pili wa maisha ya uchamungu ya Diamond.