logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Birthday ya Pritty Vishy yakosa msisimko huko akipata zawadi moja

Alionekana akilalama baada ya kupata zawadi moja kinyume na alivyokadiria.

image
na Davis Ojiambo

Burudani05 October 2022 - 06:09

Muhtasari


  • • Pritty Vishy alikuwa akisherehekea kufikisha miaka 21.
  • • Alionekana akilalama kuwa alipata zawadi moja kinyume na alivyotarajia.
Pritty Vishy sherehekea siku yake ya kuzaliwa

Siku moja kabla ya Pritty Vishy kusherehekea siku kwa kufikisha miaka 21, ameonekana kwenye ukurasa wake wa Facebook akitoa cheche za matusi kwa mashabiki wake baada ya kupata zawadi moja kinyume na alivyotarajia.

Mwanablogu huyo siku chache kabla ya siku yake ya kuzaliwa alisema kwamba  siku yake ya birthday  itakuwa sherehe ya kukata na shoka.

Mambo hata hivyo yalikuwa tofauti kwa siku yake haikuwa yenye bashabasha kama alivyokuwa amechocha. Vishy ambaye alivuma sana kutoka kwa mpenziwe wa zamani Stevo Simple Boy alisema kwamba ni watu wachache waliohudhuria hafla yake.

‘’Eii you pple unaweza kuwa mbaya kama... yani zaidi ya 500 birthday wishes then 1 zawadi eiiii haidhuru’’ Pritty Vishy alisema.

Kupitia ukurasa wa Radio Jambo shabiki mmoja alimtakia Vishy heri kwenye siku yake, mashabiki walituma jumbe nyingi na kutilia shaka umri halisi wa Vishy. Wengi walisema yu ngali mdogo licha ya mwili wake.

''Happy birthday girl enjoy your day,kwa wale mnasema hayuko 21 Kwan nyie ndio mlimzaa.stop body shaming her.kuwa na mwili kubwa haimaanishi ni mkubwa kimiaka.na nyinyi wenye mko na miili tudonye na miaka mob mnadhani nyinyi n watoi.tumwili tumekauka.nkt.achaneni na vishy'' Zulfa Mwanzi nnoja wa mashabiki aliandika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved