logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+video) Baba unanuka jasho, nenda uoge - bintiye DJ Mo amwambia

“Baba unanuka, unahitaji kuenda na ukaoge, kwa sababu unatokwa na jasho,” Ladasha Wamb0 alimwambia babake.

image
na Radio Jambo

Makala05 October 2022 - 09:11

Muhtasari


• Natoka hustle kuhakikisha anaishi maisha halafu @ladashabelle.wambo awe na ujasiri wa kuniambia ninanuka - DJ Mo.

Mcheza santuri wa muda mrefu DJ Mo amewachekesha watu kwenye mtandao wa Instagram baada ya kupakia klipu ikimuonesha bintiye Ladasha Wambo akimwambia kuwa ananuka.

Katika video hiyo, DJ Mo aliingia kweney sebule ambapo bintiye Ladasha alikuwa anatizama simu aliyokuwa akiishikilia mkononi. Mo alimwambia bintiye aende mikononi mwake ili ambebe, jambo ambalo binti mtu alikataa kwa kusema kwamba babake huyo alikuwa ananuka uvundo.

Ladasha alimtaka babake kuingia bafuni na kuoga kabla ya kutaka kumbeba kwa sababu ya kunuka kwake.

“Baba unanuka, unahitaji kuenda na ukaoge, kwa sababu unatokwa na jasho,” Ladasha Wambo alimwambia babake huku mkewe Mo, Size 8 ambaye alikuwa akirekodi video ile akicheka.

Mtoto huyo alimwambia babake kuwa alikuwa ananuka uvundo kutokana na kutokwa na jasho, jambo ambalo Mo hakulifurahia kabisa.

“Yaaani hata sinuki kitu 😂😂😂😂. .Natoka hustle kuhakikisha anaishi maisha halafu @ladashabelle.wambo awe na ujasiri wa kuniambia ninanuka 😂😂..Asante kwa kurekodi nitamkumbusha siku moja. Je, unapitia vile na watoto wako pia??” DJ Mo aliandika kwenye video hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved