(+video) Zuchu ateta paka wake kupata mimba ilhali yeye bado hajapata

Mashabiki wake walirai kukubali kumbebea Diamond Mimba badala ya kuteta kuwa hajapata.

Muhtasari

• Mwanangu vibaya hivo umenidhalilisha mpaka naonekana mama gani mimi nisiyejua kulea - Zuchu.

Msanii kutoka lebo ya WCB Wasafi Zuchu ameibuka na mapya baada ya kupakia video kwenye instastories zake akiteta vikali kuwa paka wake amepata mimba hali ya kuwa yeye bado.

Katika video hiyo amabyo Zuchu alimfananisha paka wake kama mtoto wake, anaonekana akimpapasa paka huyo kichwani huku akisema kuwa ameenda nje na kupata mimba kabla ya mamake.

“Yaani huyu paka wangu ameshaenda akatafuta wenzake wamempa mimba sasa hivi, mimi mamake sina mimba yeye tayari washampa mimba kwa nini? Mwanangu vibaya hivo umenidhalilisha mpaka naonekana mama gani mimi nisiyejua kulea,” Zuchu anasikika akiteta kwenye video ile.

Paka yule alijaribu kukwepa mikononi mwake na kumrudisha kwa kamera akisema anataka walimwengu wamuone jinsi alivyopata mimba kabla ya mama yake, ambaye katika muktadha ule alikuwa ni yeye mwenyewe Zuchu.

“Njoo huku walimwengu wakuone. Mkimkuta na wanaume huyu mmfukuze jamani,” Zuchu anamtania paka wake.

Baadhi ya watu walioona klipu hiyo waliingia mitandaoni na kumrai kukubali kumzalia Diamond Platnumz mimba.

Walikuwa wanamwambia hivyo kutokana na sekeseke za mitandanoni ambazo zimekuwa zikienezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kuhusu msanii huyo kutoka kimapenzi na Diamond Platnumz.

Hata baada ya minong’ono hiyo, hakuna hata mmoja kati ya Diamond au Zuchu ambaye alijitokeza wazi na kulizungumzia hilo la kuwa pamoja kimapenzi.

Zuchu kwa muda mrefu amekuwa akisisitiza kubaki katika njia kuu kuwa yeye kinachomfanya kuwa na ukaribu na Diamond Platnumz ni muziki tu na wala hakuna kitu kingine kwani anamheshimu na kumchukulia kama bosi wake.