Ujumbe wa Betty Kyallo kwa Vera Sidika baada ya kukejeliwa mitandaoni

"Wasichana wetu wachanga lazima wajue kwamba sio mtazamo wa watu juu yetu.

Muhtasari
  • Wanamitandao wengi walimshambulia mwanasosholaiti huyo,huku mumewe akimwandikia ujumbe wa kumtia moyo
Image: VERA SIDIKA//INSTAGRAM

Mwanasosholaiti Vera Sidika alizua gumzo mitandaoni baada kufanyiwa upasuaji,huku ukibadilisha umbo lake.

Wanamitandao wengi walimshambulia mwanasosholaiti huyo,huku mumewe akimwandikia ujumbe wa kumtia moyo.

Ni gumzo ambayo haikumuacha Betty KYallo nyuma kwani alimtumia Vera ujumbe wa kumtia moyo.

Baada ya kauli yake, Bi. Kyallo alimtia moyo kamwe asiepuke kuishi ukweli wake na akamsifu kwa kuwa jasiri kushiriki safari yake.

"Unastahili kuishi ukweli wako. Unastahili maisha yenye afya na furaha kwa jambo hilo. Ninakupigia makofi kwa kuwa jasiri," alisema.

Betty aliongeza;

"Wasichana wetu wachanga lazima wajue kwamba sio mtazamo wa watu juu yetu. Jinsi tunavyoonekana, mavazi, na jinsi tulivyo nene au nyembamba, iwe ngozi nyepesi au nyeusi. Wanapaswa kujua kamwe kutoa mamlaka kwa wageni juu ya jinsi wanapaswa kujisikia. kuhusu wao wenyewe,”.

Katika chapisho la hivi majuzi kwenye mtandao wake wa Instagram, Vera alichapisha kipande cha utaratibu huo huku akiwaahidi mashabiki wake kuwa ataweka wazi video nzima mitandaoni.

"Kama uko hai na u mzima. Asante Mungu. Usiichukulie poa. Nilipewa nafasi ya pili ya kuanza upya, na kubaki hai kabla hali haijawa mbaya zaidi. Huenda nisiwe na mwili ambao umezoea kuuona lakini Niko hai na hakuna kinachoshinda hivyo."