Wanawake maarufu waliofanyiwa upasuaji wa kubadilisha mwonekano wa miili yao

Upasuaji wa kupunguza mafuta mwilini unaitwa liposuction

Muhtasari

• Vera alifanyiwa upasuaji wa kuongeza  matiti, makalio na pia kubadilishwa rangi ya ngozi ili awe mweupe.

Vera Sidika//Jackie Matubia//Yummy Mummy

Wanawake maarufu waliofanyiwa upasuaji wa mwili, kila mmoja akiwa na nia yake tofauti ya kufanyiwa upasuaji huo.

Wengine waliofanyiwa upasuaji wa mwili ili kupunguza mafuta ya mwili huku wengine wakafanyiwa ili kuongeza viuongo vya mwili ambavyo walitamani viwe umbo fulani.

Upasuaji wa kupunguza mafuta mwilini unaitwa liposuction. Upasuaji huu unapunguza mwili kwa kumfanya mtu apunguze kiwango cha chakula anachokula kwa siku.

Miongoni mwa wanawake maarufu ambao wamefanyiwa upasuaji wa kimwili ni:

Vera Sidika

Vera alifanyiwa upasuaji wa kuongeza  matiti, makalio na pia kubadilishwa rangi ya ngozi ili awe mweupe. Pia amefanyiwa upasuaji wa kuyapunguza makalio baada ya kumletea shida za kiafya.

Mwanaosholaiti huyo anajulikana kwa viuongo vyake vya kike vinavyowavutia mashabiki wake.

Yummy Mummy

Mwanablogu wa YouTube Murugi Munyi almaarufu Yummy Mummy pia alifanyiwa upasuaji wa mwili wake ili kuupunguza, upasuaji huo kwa kimombo ni liposuction.

Munyi alifanyiwa upasuaji huo baada ya kujifungua na kuongeza mwili kwa kunenepa .

Huddah Monroe

Mwanasosholiti huyo alifanyiwa upasuaji wa mwili wa kuongeza matiti ila aligeuka na kurudisha mwili wake wa zamani kwa kutoa matiti bandia.

Kisa cha kutoa matiti hayo bandia kilitokea baada yake kupata shida za kiafya.

Risper Faith

Alifanyiwa upasuaji wa liposuction ili kupunguza mafuta kwenye mwili wake. Baada ya upasuaji huo Risper alipunguza mafuta na kupata umbo aliokuwa anataka.

Jackie Matubia

Mwigizaji huyu pia alifanyiwa upasuaji wa kupunguza mafuta mwilini miezi baada ya kujifungua na kuongeza mwili.

Alisema kuwa alipunguza kilo sita kabla wiki iishe baada ya kufanyiwa upasuaji huo.

Cathrine Kamau

Aliyekuwa mwigizaji wa Tahidi High alifanyiwa upasuaji wa kupunguza mwili wake baada ya kujifungua mtoto wake wa pili na kuongeza mwili.