Mwanamuziki Jovial na mpenzi wake Willy Paul wameendelea kuonyesha mahaba yao hata baada ya kuutoa wimbo wao wa lalala.
Kulingana na ujumbe kwenye Instagram , wanamitandao walikuwa wamesingizia uhusiano wao kuwa kiki.
Mpenzi huyo wa Willy Paul aliweka kwenye ukurasa wake wa Instagram picha yake akiongelea jinsi uhusiano wake na msanii huyo anaendelea munoga.
"Kama michirizi ya maji, mapenzi yanatiririka mwilini mwangu,"mwanamuziki huyo alisema.
Willy Paul alijibu kwenye ujumbe huo akisema kuwa anachofanyiwa na Jovial ni yeye pekee anajua.
"Wacha niende na mwendo wa kasi ya 40 basi," Jovial alimjibu.
Katika msururu wa maswali na majibu kwenye ukurasa wake wa Instagram, Jovial aliulizwa ilikuwaje akakubali kuingizwa 'box' na Willy Paul hata baada ya kusema hawezi kuwa mpenzi wa Willy Paul kwa sababu 'ana utoto'.
Jovial alisema kuwa alijipa muda kumfahamu vyema Willy Paul na aligundua kuwa mwanamuziki huyo ni mtu mzuri na mwenye roho safi licha ya watu kumwagia tope sifa zake.
Aliongeza kuwa Willy Paul ni mtu anayejali watu wa karibu naye, lakini kama mtu yoyote yule ana mapungufu yake na ni msumbufu.
"Ni kichwa ngumu tu ndio ako nayo, lakini uzuri ni kuwa amepata kichwa bangi, mimi sasa ndio kichwa mbaya,nilipenda roho yake."alisema.
Jovial alisema kuwa kitu cha muhimu kwenye uhusiano ni kuelewana na mpenzi wako ili kufahamu njia nzuri ya kuishi naye bila utata wowote.
"Kila mtu ako na dosari na kama ni mabadiliko myafanye pamoja ,"alisema.
Jovial na Willy Paul wametangaza kuwa kwenye mahusiano kwa takriban wiki tatu sasa na hata baada ya watu kutarajia kuwa wataachana baada ya kutoa wimbo wao lakini mapenzi yamenawiri.