logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+video) Nyashmentation: Wanunu adhibitisha makalio yake si feki

“Kuwadhibitishia tu kwamba yangu ni ya kiasili kabisa, Nyashmentation,” Mary Wanunu aliandika kwenye video hiyo.

image
na Radio Jambo

Habari07 October 2022 - 09:22

Muhtasari


• Alhamisi pia Lady Risper naye alibainisha kuwa yake ni ya kiasili na kuwataka wale wanaomsema kuwa atafuata Sidika kukoma.

Afisa maarufu kutoka idara ya magereza Mary Wanunu amepakia video yake akisema ni kudhihirishia watu na mashabiki wake kuwa makalio yake si bandia bali ni ya kiasili.

Kupitia Instagram yake, Wanunu alipakia video hiyo na kusema ni kudhibitisha tu kwa watu ambao wameanza kushuku makalio yake kuwa huenda si halisi, haswa baada ya mwanasosholaiti mstaafu Vera Sidika kuzua mjadala huo alipofanyiwa upasuaji wa kuondoa makalio feki aliyokuwa nayo kwa muda mrefu.

Wanunu alipakia video hiyo inayomuonesha mduara mzima jinsi anajigeuza ili kudhibitishia watu kuwa yake ni ya kurubuni.

“Kuwadhibitishia tu kwamba yangu ni ya kiasili kabisa, Nyashmentation,” Mary Wanunu aliandika kwenye video hiyo.

Haya yanakuja siku chache tu baada ya wanasosholaiti kuanza kutupiwa maneno kuwa huenda pia wanabeba makalio ya kuwekewa kupitia upasuaji na si yao kiasili.

Juzi Vera Sidika alipakia picha yake mpya bila makalio akisema kuwa iimbidi kufanyiwa upasuaji ili kurudisha hali yake ya kawaida baada ya upasuaji wa kuongeza makalio kumwendea mrama, kile alichokieleza kuwa alinusurika kifo.

 Sidika pia aliwashauri wanadada kujipenda na kujikubali jinsi walivyo na makalio yao ya viwango tofauti pasi na kuingiwa na kile alichokiita pepo ya kutaka kufanya upasuaji ili kuongezwa, akisema madhara yake ni makubwa na mazingo kama nanga.

Mwanasosholaiti Lady Risper pia alipakia picha yake siku moja baadae na kusema makalio yake si ya kubandikiwa kupitia upasuaji.

Lady Risper aliwaambia watu kukoma kurundika kwenye DM yake kumwambia kwamba akiona kichwa cha Sidika kimenyolewa basi yeye ndiye atakayefuata na kujiweka tayari.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved