logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Uko na wa kukuangalia hivi ama bora uhai?" Dorea Chege awatania watu na picha yake na Dibul

“Lakini si @dj_dibul unaskianga fiti,” Dorea Chege aliandika.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri08 October 2022 - 12:07

Muhtasari


• “Uko na wa kukwangalia hivi ama bora uhai?” Dorea alitania.

Dorea Chege na mpenzi wake DJ Dibul

Aliyekuwa mwigizaji katika kipindi cha runinga cha Maria, Dorea Chege almaarufu Maggie amejisifia kwa mpenzi wake mcheza santuri DJ Dibul.

Katika picha ambayo mwigizaji huyo alipakia akiwa na ulimbwende wa aina yake, alijisifia kwa kudokeza kwamba yeye ni kila kitu amabcho mwanaume yeyote hawezi taka kukipoteza maishani.

Alimtania mpenzi huyo wake kuwa huwa anajihisi vizuri sana kila mara anapokuwa na yeye.

Lakini si @dj_dibul unaskianga fiti,” Dorea Chege aliandika.

Dorea na mpenzi wake wanaendeleza ujenzi wa jumba lao la kifahari amablo wamekuwa wakionesha wanamitandao katika kila hatua.

Mwigizaji huyo alifunguka kuwa marafiki wake karibia wote walimtoroka pindi tu alipoanzisha mjengo wake huku wakifikiria kwamba angeanza kuwa omba omba kwao kutokana na gharama zilizokwea za bidhaa za ujenzi.

DJ Dibul na Dorea Chege wamekuwa ni wapenzi wa kuonesha mahaba yao mitandaoni bila kuogopa huku wakipakia kumbukumbu katika picha wakiwa wanakula bata katika sehemu za kifahari ndani na nje ya Kenya.

Dorea kwa wakati mmoja aliwatania mashabiki wake kwa kutaka kujua kama wana mtu wa kuwatazama kwa mahaba kama alivyokuwa ametazwa na mpenzi wake katika moja ya picha.

“Uko na wa kukwangalia hivi ama bora uhai?” Dorea alitania.

Mwigizaji huyo mapema mwaka huu alikuwa na azimio la kuwania wadhfa wa mwakilishi wa kike Nairobi, azma ambalo haijulikani nini kilitokea na hakuonekana tena kwenye kampeni wala kufika debeni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved