logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hangaika tu na bado hujanipa mapacha! - Nandy amtania mumewe, Billnass

Unajua bado hujanipa mapacha eeeeeee!!!!! We hangaika tu - Nandy.

image
na Radio Jambo

Makala09 October 2022 - 05:12

Muhtasari


• Kwa utani wake, Nandy alikuwa anamwambia Billnass kutofurahia sana kwani bado ana deni la mapacha kwa mkewe.

Nandy amwambia Billnas bado hajampa mapacha

Mwanamuziki Nandy amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupakia picha ya bwanake, Billnass akiwa akajivinjari kwa kupepea juu ya bahari na parachute.

Katika picha hiyo, Billnass alionekana akijiburudisha kwa kupaa na kupepea juu ya bahari kwa kutumia parachuti, kitu ambacho wengi wanaogopa sana kufanya kutokana na woga wa kutazamana moja kwa moja na kina kirefu cha maji au hata kuning’inia kwenye parachuti kwa futi kadhaa za kuhesabu kutoka ardhini.

Nandy kwa mzaha, alionekana kumtahadharisha Billnass kutoshiriki katika mchezo kama huo hatari ambao huenda parachuti ile ikifeli atazama kwenye bahari hiyo hali ya kuwa bado hajampa mapacha.

Alimwambia kwamba licha ya kuhangaika kujipa raha kwa kupepea kwa chombo hicho lakini anafaa kuweka kichwani mwake kwamba ana deni kubwa kwa mkewe Nandy ambalo ni sharti alitimize – deni la kumzalisha watoto mapacha!

Unajua bado hujanipa mapacha eeeeeee!!!!! We hangaika tu!!!! Sema nimetamani..😋😋 @billnass,” Nandy alimtania huku mwisho akisema kuwa hata yeye ametamani kushiriki mchezo ule wa kujiburudisha kwa parachuti angani.

Wanamitandao wengine walimsihi Nandy kupakia picha ya mtoto wao angalau wamuone.

Ikumbukwe alipokuwa anakaribia kujifungua, Nandy katika mahojiano na wanahabari akizindua Nandy Festival alisema kwamba hakuna mtu atakayekuja kumuona mtoto wake akiwa mdogo haswa kwenye mitandao ya kijamii.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisema kuwa hawezi kufuata upepo na kurubuniwa kumfungulia mwanawe akaunti kwenye mitandao ya kijamii, mpaka pale atakapokuwa mkubwa na kujifanyia maamuzi hayo mwenyewe.

Aidha, alisema kuwa hawezi hata fichua jinsia ya mwanawe kwa jamii ya mitandaoni, wala sura na jina vitabaki siri yao kama wazazi na hata ncha hawatowashirikisha wanamitandao katika makuzi ya mtoto.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved