Vera Sidika ajitetea kutumia upasuaji wa makalio yake kutafuta kiki kwa ajili ya ngoma yake

Sidika aliwataka wale wanaoona alifanya vibaya kufukuzia kiki kumtafuta na kubusu makalio yake.

Muhtasari

• Nyinyi wote hamkuona kuwa la umuhimu wowote wakati watu walikuwa wakinidhihaki, wakinicheka kwa kuwa na matatizo kutokana na upasuaji - Vera Sidika.

Vera awajibu wanaomkejeli kwa kiki
Vera awajibu wanaomkejeli kwa kiki
Image: instagram

Kama kuna mtu ambaye aliwapata mashabiki pasi na kujipanga kwa kufukuzia kiki mitandaoni basi ni mwanasosholaiti mstaafu Vera Sidika.

Baada ya kutrend kwenye mitandao kutokana na madai ya kufanya upasuaji wa kupunguza makalio kwa kile alisema ni sababu za kiafya, mwanadada huyo kwa mara nyingine tena anazidi kushikilia chati za kuzungumziwa sana mitandaoni.

Safari hii gumzo kubwa ni jinsi alivyowapiga change la macho watumizi wa mitandao kwa kuwahadaa kwamba amefanya upasuaji wa kupungumza makalio kumbe ilikuwa ni uongo tu wa kutafuta kiki kwa ajili ya wimbo wake mpya wa Popstar.

Na lazima tukubali, ugumu wa mshikamano ulitupata bila kujua. Ukweli kwamba mumewe Brown Mauzo pia alijiunga na ulaghai ulioratibiwa kwa siri ulitufanya tumwamini hata zaidi.

Vera pia alipakia video ambayo iliaminika kuwa ya utaratibu wake wa kupunguza makalio na kuilifanya sakata zima kuonekana kuwa la ukweli kabisa kumbe maskini wa Mungu tulikuwa tunachezwa kama mpira wa kitenesi.

Baada ya kuachia wimbo wake na kugundulika kwamba alikuwa anatafuta kiki na ukweli kubainika kuwa hakufanya upasuaji wa kupunguza makalio, Msanii huyo mpya alijipata katika majibizano makali na baadhi ya wanamitandao waliomsuta kwa kuwapiga changa la macho na kuwaharibia muda kumzungumzia mitandaoni.

Sidika sasa ameamua kuweka ukimya pembeni na kujibwaga kwenye ulingo wa vita vya maneno dhidi ya watu hao ambapo amewasuta kwamba walikuwa wanafurahi akisimangwa kuwa amefanya upasuaji na baada ya kugundua kuwa haukuwa ukweli sasa wanamtukana.

Sidika aliwanyamazisha kwa maneno na cheche kali zisizoweza kutamkika mbele ya kadamnasi.

“Nyinyi wote hamkuona kuwa la umuhimu wowote wakati watu walikuwa wakinidhihaki, wakinicheka kwa kuwa na matatizo kutokana na upasuaji. Hata mlijiunga nao kunikejeli. Na mlifurahia. Lakini sasa mnaona ni muhimu sana kwamba ilikuwa kiki tu. Kwa hivyo ni sawa kwako kucheka shida / hali yangu na sio kinyume chake. Lmaoo, nyote mnaweza kubusu makalio yangu yaliyopauka,” Sidika aliwatupia bomu la moto wakosoaji wake.