logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilimpenda Kawira kwa moyo wangu wote, nimetattoo majina ya watoto mkononi - Ephantus Safari

Nilimpenda Joy kwa moyo wangu wote. Nimeandika herufi za kwanza za watoto wangu kwenye mkono wangu - Ephantus.

image
na Davis Ojiambo

Burudani11 October 2022 - 07:06

Muhtasari


  • • Mwanaume huyo alieleza kwa uchungu kwamba madai ya Kawira kuwa alikuwa mnyanyasaji yamemchafulia jina vibaya sana.
Ephantus Safari afunguka kilichosababisha ndoa yake na Joy Kawira kugonga mwamba

Aliyekuwa mume wa mwigizaji wa Papa Shirandula Joy Kawira hatimaye amefunguka kuhusu madai ambayo mwigizaji huyo anazidi kumlimbikizia katika mahojiano na vituo mbali mbali kuhusu kuvunjika kwa ndoa yao ya miaka 6.

 Ephantus Safari amabye ni mzalishaji wa miziki ya injili kwa muda mrefu amekuwa si mtu wa kuzungumza sana kuhusu kuvunjika kwa ndoa yao. Kwa upande wake, Kawira ambaye alikuwa mke wake amekuwa mtu wa kufunguka sana kuhusu kilichosababisha ndoa yao kuvunjika.

Ikumbukwe katika mahojiano na mtangazaji wa Radio Jambo, Massawe Japanni wiki mbili zilizopita, Kawira alifunguka kwamba mumewe huyo alikuwa mnyanyasaji katika ndoa ambapo alisema alikuwa anamdunda kama ngoma kila wakati.

Ephantus kupitia ukurasa wake wa Facebook, aliachia ujumbe mrefu wa kuelezea matukio yaliyojiri mpaka kusambaratika kwa ndoa yao na Kawira.

Katika maelezo hayo marefu, Ephantus alieleza jinsi alitembea katika safari yenye ugumu na mkewe huku akisema kuwa matatizo yalianza pale Kawira alipomruhusu mamake mzazi kuishi katika nyumba yao.

Pia alieleza jinsi alizidi kumpa moyo wakati wa kipindi kigumu cha kutopata mtoto na mpaka kumrai kutafuta suluhu kwa daktari ambapo hatimaye alifanikiwa kupata ujauzito amabo walilazimika kuukatisha kutokana na sababu za kiafya.

Aidha, pia walizidi kuomba na baadae tena mkewe akapata ujauzito wa mapacha watatu ila baada ya wiki kama 32, daktari aliwaarifu kuwa mtoto mmoja ameaga tumboni jambo ambalo lilisababisha watoto wawili kuokolewa na kulelewa katika njia maalumu kabla ya kufikisha muda stahili wa kuzaliwa.

Ephantus alisema kuwa amekuwa akipitia wakati mgumu sana kwa kutoruhusiwa kuwaona wanawe ambapo ilimbidi mpaka kuweka herufi za majina yao kweney mwili wake.

“Niliiweka familia yangu katika hali bora kabisa ambayo mwanaume anaweza kumuweka mwanamke. Nilihudumia familia yangu hadi kufikia hatua ya kutegemeza familia kubwa pia lakini jioni moja kutoka kazini nilipata nyumba tupu. Nilimpenda Joy kwa moyo wangu wote. Nimeandika herufi za kwanza za watoto wangu kwenye mkono wangu,” Ephantus Safari alisimulia.

Mwanaume huyo alieleza kwa uchungu kwamba madai ya Kawira kuwa alikuwa mnyanyasaji yamemchafulia jina vibaya sana.

“Shutuma zake zimeharibu sifa yangu. Biashara zangu zinafeli. Inauma, anapata faraja hizi zote kutoka kwa mtu niliyemwita 'mama'; ‘mama’ ambaye alikuwa akipinga mimi kumuoa tangu siku nilipomtambulisha,” Ephantus alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved