Nilienda kwa Harmonize nikamkuta na boxer na Paula anampapasa kifuani - Mwijaku

Mwijaku alikuwa anatoa maelezo haya katika kituo cha ustawi bora kwa jamii akilenga kumshtaki Harmonize kwa kumdhulumu Paula.

Muhtasari

• Nikamwambia hii sio sawa akaniambia haya ni mambo ya kifamilia yaache, akasema Pesa inaoongea - Mwijaku.

Mwijaku aibuka na jipya kuhusu Mahusiano ya Kajala bintiye Paula na Harmonize
Mwijaku aibuka na jipya kuhusu Mahusiano ya Kajala bintiye Paula na Harmonize
Image: Instagram

Mtangazaji Mwijaku amezidi kumchimba mikwara msanii Harmonize kwa tuhuma za kutoka kimapenzi na Kajala Masanja pamoja na bintiye Paula Kajala kwa zamu.

Mwijaku alichukua hatua zaidi na kuenda mpaka kituo cha ustawi wa jamii kumshtaki Harmonize akitaka achukuliwe hatua za kisheria kwa kile alisema kwamba anamdhulumu Paula ambaye ni mtoto.

Kulingana na Mwijaku, Paula ni mtoto mdogo na anachopitia mikononi mwa Harmonize ni dhuluma za kimapenzi ambapo Harmonize anawatumia wote binti na mama kimapenzi.

Mwijaku alielezea kwamba Kajala mwenyewe amenyamazia suala hilo la Harmonzie kumtumia bintiye pia kimapenzi kutokana na ugumu na changamoto za kifedha ambazo zinawafanya wawili hao kuridhia kulala pamoja na msanii Harmonize.

Mtangazaji huyo hata alizidi kuelezea kwamba ana ushahidi mtupu wa kile alichokuwa akisema na kusimulia kuwa kwa wakati mmoja alitembelea familia hiyo na kuona jinsi Harmonize alivyokuwa anamfanyia Paula kutokana na ugumu wake wa kifedha.

Siku moja nilienda kwa Harmonize nikamkuta sebuleni amekaa na Boxer halafu Paula anampapasa kifuani mimi kama Mzazi sikupenda nikamwambia hii sio sawa akaniambia haya ni mambo ya kifamilia yaache, akasema Pesa inaoongea,” Mwijaku alisema.

Mwijaku alisema kuwa ni dhambi kubwa kwa Harmonize kutumia kigezo cha kuwa na pesa kwa kuwadhulumu Kajala na bintiye kimapenzi.

Awali mtangazaji huyo aliibua madai kwamba duka la nguo la Paula alimfungulia yeye na ndio maana amemrudisha kimawasiliano na hata kumfanya Paula kumkubali kama baba yake wa kambo, kinyume na awali amabpo binti huyo wa Kajala alikuwa hampendi kabisa Harmonize kutokana na sakata la awali la kumtumia picha za utupu wake.