logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Kuna Opaqueness": Drake, The Weeknd kususia tuzo za Grammy kwa mara nyingine tena

Wawili hao walioongoza chati zote hapo awali walitangaza wasiwasi wao kuhusu jinsi mambo yanavyofanya kazi nyuma ya pazia.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri17 October 2022 - 11:40

Muhtasari


• Angalia, mimi binafsi sijali tena. Nina Grammys tatu, ambazo hazina maana kwangu sasa, ni wazi - The Weeknd.

The Weeknd na Drake wakwepa tuzo za Grammy

Wasanii maarufu duniani kutoka taifa la Canada, Drake na The Weeknd wametangaza kutohudhuria hafla ya tuzo maarufu duniani za Grammy ambazo zitafanyika mwaka kesho.

Hii ni mara ya pili kwa wakali hao kuipa mgongo hafla hiyo ya tuzo za Grammy na kulingana na jarida la Mirror, wasanii hao wamechagua kutowasilisha kazi zao zozote kwenye wasimamizi wa tuzo hizo.

Wawili hao walioongoza chati zote hapo awali walitangaza wasiwasi wao kuhusu jinsi mambo yanavyofanya kazi nyuma ya pazia na shirika lililo nyuma ya sherehe hiyo ya kifahari.

Sifa hizo zinazotamaniwa sana ni miongoni mwa zile zinazotafutwa sana katika biashara hiyo, lakini hilo halijamzuia Drake, 35, na The Weeknd mwenye umri wa miaka 32 kulipa kisogo tukio hilo.

The Weeknd - jina halisi la Abel Makkonen Tesfaye - alitangaza kwa mara ya kwanza uamuzi wake wa kususia hafla hiyo mnamo 2021 wakati albamu yake ya 2020 After Hours ilipopigiwa kelele ya kukataliwa, licha ya kuwa maarufu sana kwa wakosoaji.

Msanii huyo alisema kwamba katika maisha yake tayari ameshinda tuzo za Grammy mara tatu na ambazo hazimsaidii kitu na kusema haoni haja ya kushiriki tena.

“Angalia, mimi binafsi sijali tena. Nina Grammys tatu, ambazo hazina maana kwangu sasa, ni wazi. Hata hivyo mimi hujivunia kutoa hotuba. Sahau maonyesho ya tuzo,” The Weeknd alinukuliwa na jarida hilo.

Wakati huohuo Drake amekuwa na matatizo na Grammys tangu 2017 alipopewa sifa ndogo zaidi kwa wimbo wake wa Hotline Bling - ambao uliteuliwa kuwania Utendaji Bora wa Rap/Sung na Wimbo Bora wa Rap.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved