Eric Omondi afunguka kuhusu uhusiano wake wa sasa na Jacque Maribe

Omondi alisema kuwa yeye huwasiliana mtoto wa Maribe na kumjulia hali mara kwa mara.

Muhtasari

• Omondi alisema yeye na Maribe huwasiliana anapokuwa akizungumza na mtoto na kuweka wazi kuwa wana urafiki wa karibu.

•Aliongeza hata kabla ya kusuluhisha mzozo uliopo bado hana shida kutekeleza wajibu wake wa kuwa na uhusiano na mtoto huyo.

Eric Omondi na Jacque Maribe

Aliyekuwa mchekeshaji wa Churchill, Eric Omondi amefichua kuwa yeye na anayedaiwa kuwa mzazi mwenzake ,Jacque Maribe, wana uhusiano wa karibu.

Katika mahojiano na Mwende Macharia, Omondi alisema kuwa yeye huwasiliana mtoto wa Maribe na kumjulia hali mara kwa mara.

Pia alisema yeye na Maribe huwasiliana anapokuwa akizungumza na mtoto huyo na kuweka wazi kuwa wana urafiki wa karibu. 

"Nilishauriwa niache kuongelea mambo ya mtoto.Najuta sana, hasira hasara, nilikuwa nasema mambo ya kweli ya maisha yangu, nilijuta baadaye.  Nina uhusiano mzuri na mtoto huyo na hata mama yake," Omondi alisema.

Omondi alisema kuwa aliamua kunyamazia suala hilo ili kuzuia kumwingiza mtoto kwenye masuala ya watu wazima.

Alisema kuwa watu walipoanza kutoa maoni kuhusu mtoto huyo, alitaka kufanya suala hilo lididimie ili wanamitandao wanyamaze.

Aliongeza kuwa hata kabla ya kusuluhisha mzozo uliopo bado hana shida kutekeleza wajibu wake wa kuwa na uhusiano na mtoto huyo.

Mtumbuizaji huyo alisema kuwa hata bada ya kutaka kuangazia sheria na kufikisha suala hilo mahakamani aliamua kulipuuzila mbali.

"Hatukusuluhisha , niliambiwa nimnyamazishe na kuwa nisiyaongelee maneno hayo. Wanablogu walikuja nikaona nikiendelea kuongea mtoto atazingatiwa na hayo si mambo mazuri," Omondi alieleza.

Alisema kuwa alinyamaza na baada ya hapo alijaribu kusafisha jina lake lililokuwa limechafuliwa kwa maneno mabaya kuhusu suala hilo.

"Nilikuwa nataka kujiosha kwa kuwa nilikuwa nimetupiwa matope, sikutaka kumwingiza mtoto kwenye saga hiyo chafu. Katika harakati hiyo nilisema mambo yangu ya kindani,nilikuwa nimekasirika lakini najuta sana," aliongeza.