Mwanzo mpya! Msanii Vivianne anyoa nywele baada ya kutengana na mumewe

Msanii huyo alipakia picha akiwa na upara na kusema kwamba alilazimika kuanza upya kimaisha.

Muhtasari

• Badala ya kutafuta faraja ya kidunia Mungu alinilazimu nimtamani Yeye. Ilikuwa ni ajabu sana. - Vivianne.

Vivianne na muonekano mpya baada ya kuvunjika kwa ndoa yake
Vivianne na muonekano mpya baada ya kuvunjika kwa ndoa yake
Image: Instagram

Miezi michache iliyopita, msanii wa kizazi kipya nchini Kenya, Vivian alivumishwa kuwa aliachana na meneja wake ambaye pia alikuwa mume wake  Sam West juu ya tofauti zisizoweza kusuluhishwa.

Yote yaligeuka kuwa kweli baada ya kuvunja ukimya wake wiki kadhaa baada ya uvumi huo. Wanandoa hao walikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliopendwa na wengi kwa familia yao iliyochanganyika, kila mmoja akiwa na mtoto kutoka kwa uhusiano wa awali.

Baada ya kimya kirefu, msanii huyo Ijumaa iliyopita aliweka wazi kupitia kurasa zake mitandaoni kuwa hayuko sawa na anapitia wakati mgumu sana kutokana na matukio yaliyokuwa yakiendelea katika maisha yake – matukio ambayo yalihusishwa na kusambaratika kwa uhusiano wake na Sam West.

“Siko vizuri, nimekuwa nikipata msaada lakini wakati mwingine naanguka. Moyo wangu ni mzito sana. Mtu alituacha na sasa anatuchukia. Nimekuwa nikijaribu kujenga upya lakini nimekuwa nikijiuliza kwanini. Tafadhali niombee kwa sababu mimi bado ni mama,” Vivianne aliandika.

Baadae msanii huyo alipakia picha kwenye Instagram yake akiwa na muonekano mpya kabisa bila nywele hata kidogo. Huku akidokeza kwamba hatua yake kuzitupilia mbali nywele ni kama kuanza upya maisha.

“Nilitambua kwamba haijalishi nilifanya nini au nilisema nini na jinsi sikuwa tayari kwa mabadiliko katika maisha yangu kwamba ilikuwa juu ya uwezo wangu kabisa. Kwa hiyo badala ya kutafuta faraja ya kidunia Mungu alinilazimu nimtamani Yeye. Ilikuwa ni ajabu sana. Na siku hizo mimi hukata tamaa juu ya maisha yangu ya zamani, malezi yangu na maumivu mengine najilazimisha kuhamisha zingatio langu,” Vivianne aliandika kwenye picha hiyo mpya.