Eric Omondi awaonya mapromota dhidi ya kuwaleta wasanii wa nchi za kigeni

Hata hivyo, baada ya kufanya malipo ya takriban Ksh40,000 hakusikia lolote kutoka kwake.

Muhtasari
  • Amekwama Nairobi kwa muda wa mwezi mmoja uliopita na amelimbikiza madeni mengi ambayo hawezi kulipa
  • Eric Omondi amesema anamfahamu promota huyo na sasa anataka ajitokeze kumsaidia mwanadada huyo kurejea Afrika Kusini kwa kumlipa
Image: Eric omondi Instagram

Mcheshi Eric Omondi amekasirika baada ya promota mmoja kudaiwa kumlaghai Mwanamke wa Afrika Kusini na kumwacha amekwama nchini Kenya.

Katika video aliyoshiriki mchekeshaji huyo kwenye mitandao yake ya kijamii, mtayarishaji huyo alimwambia mwanadada huyo kuwa anaweza kupewa nafasi ya kutumbuiza nchini Kenya na kulipwa.

Alikubali hila hiyo na akamtumia pesa za tikiti yake na uhifadhi mwingine.

Hata hivyo, baada ya kufanya malipo ya takriban Ksh40,000 hakusikia lolote kutoka kwake.

Amekwama Nairobi kwa muda wa mwezi mmoja uliopita na amelimbikiza madeni mengi ambayo hawezi kulipa.

Eric Omondi amesema anamfahamu promota huyo na sasa anataka ajitokeze kumsaidia mwanadada huyo kurejea Afrika Kusini kwa kumlipa.

Aliendelea kumwambia kwamba ana saa sita tu za kuwasiliana na bibi huyo na kupanga safari yake ya kurejea Afrika Kusini na kama sivyo atamtafuta yeye binafsi na kuhakikisha anakamatwa.

“Mwizi aliyemleta mwanamke huyu Kenya na kumuacha hapa kwa takriban miezi miwili ana saa sita za kumpigia simu, kumlipia gharama, kumlipa na kumpatia tiketi ya ndege ya kwenda Afrika Kusini,” Eric alisema.

Pia alitoa onyo kwa mapromota wa kenya dhidi ua kuwaletea wasanii wa nchi zingine, kwa kile alichokisema kwamba hilo ni kudhoofisha usanii wa wasanii Wakenya.

"Hili ni AGIZO LANGU kwa MAPROMOTA wote katika Nchi hii!!! USITENDE!!! na narudia msiwaalike tena Wasanii wa Kigeni mpaka tupate Utaratibu. Kwanza mnaua vya kwetu halafu pili mnatutia aibu Ughaibuni!! USITENDE!!! Na ukijaribu nitahakikisha TUKIO lako halitafanyika!!! NIJARIBU WAJINGA😡😡😡😡 NIJARIBU!!!" Aliandika Eric.