Vera Sidika amsherehekea mwanawe anapohitimu mwaka 1

Vera alifichua jinsi anavyompenda Asia na vile alibadilisha maisha yake.

Muhtasari
  • "Mpendwa wangu @princess_asiabrown Ninamshukuru sana Mungu kwamba Alinichagua kuwa Baba yako. Hakuna upendo mkubwa zaidi. Heri ya kuzaliwa kwa mara ya kwanza, binti πŸŽ‚β€οΈπŸ˜˜πŸ’."
VERE SAIKIKA NA MWANAWE ASIA BROWN
Image: VERA SIDIKA/INSTAGRAM

Mjasirimali,mwanasoholaiti maarufu na mwenye utata nchini Vera Sidika amemnakilia mwanawe ujumbe wa kipekee huku akisherehekea siku yake ya kualiwa.

Mwanawe Vera Sidika na Brown Mauzo anahitimu mwaka mmoja hii leo.

Vera alifichua jinsi anavyompenda Asia na vile alibadilisha maisha yake.

Huu hapa ujumbe wake kwa mwanawe;

"@princess_asiabrown tangu siku ulipoingia katika ulimwengu huu, ulitawala moyo wangu wote na hisia hiyo imeongezeka tangu wakati huo. Nina upendo mwingi kwako, mpenzi. Huenda usitambue sasa lakini katika miaka ijayo, utatazama nyuma katika hatua hii ya awali ya maisha yako na kuona jinsi ulivyopendwa! Heri ya siku ya kuzaliwa mapigo ya moyo wangu β€οΈπŸŽŠπŸ’ƒπŸΌπŸ₯°,"Vera Aliandika.

Kwa upande mwigine mumewe Vera Sidika Brown Mauzo alimshukuru Mungu kwa kuwa baba ya Asia.

"Mpendwa wangu @princess_asiabrown Ninamshukuru sana Mungu kwamba Alinichagua kuwa Baba yako. Hakuna upendo mkubwa zaidi. Heri ya kuzaliwa kwa mara ya kwanza, binti πŸŽ‚β€οΈπŸ˜˜πŸ’."