Bintiye mwigizaji tajiri Jackie Chan aonekana akipanga foleni kupewa chakula cha msaada

Inaarifiwa kwamba binti huyo walitengana na babake na akatorokea Kanada ambako anaishi maisha ya umaskini mno.

Muhtasari

• Inaarifiwa kwamba binti huyo alilazimika kutafuta chakula cha msaada baada ya kuzidiwa na makali ya njaa licha ya babake kuaminika kuwa tajiri wa kuokotwa.

Jackie Chan ni tajiri mkubwa ila bintiye ni mtu wa kuomba omba tu
Jackie Chan ni tajiri mkubwa ila bintiye ni mtu wa kuomba omba tu
Image: Screengrab, Instagram

Katika mazingira ya kawaida, ukiambiwa kuwa mtoto wa tajiri anaeza ishi maisha ya uhayawinde, si rahisi kukubali, lakini ndio hali halisi ambalo ilitokea kwa binti wa mwigizaji maarufu duniani, Jackie Chan.

Jarida la Standard la huko Hong Kong, Etta Ng Chok-lam ambaye ni binti wa Mwigizaji huyo nguli katika filamu za mapigano, alionekana akipanga foleni kutafuta chakula cha bure huko Toronto.

Inaarifiwa kwamba binti huyo alilazimika kutafuta chakula cha msaada baada ya kuzidiwa na makali ya njaa licha ya babake kuaminika kuwa tajiri wa kuokotwa.

Jarida hilo lilitaarifu kwamba Picha za binti huyo zinazosambaa mtandaoni zilionyesha alikuwa akipanga foleni kutafuta chakula cha bure na baadhi ya wanawake wazee.

Mikononi, aionekana na mfuko mkubwa wa plastiki ambao inaaminika ndio alinuia kutumia kubebea chakula hicho cha msaada pindi baada ya kukabidhiwa.

“ Akiwa amevalia kanzu ndefu na suruali ya pamba, na viatu vichafu, Ng alionekana kutoridhika na hakuwa na roho nzuri na baadhi ya watumiaji wa mtandao walisema alionekana kama mtu asiye na makazi. Mmoja alisema binti wa mwigizaji huyo alikuwa akitafuta riziki kwa kufanya kazi katika mkahawa mmoja huko Chinatown huko Toronto,” The Standard waliripoti.

Picha hizo zinasambaa mtandaoni huku kukiwa na mradi mpya wa Chan, ambao mwigizaji huyo anasemekana kutarajia kupokea mamia ya mamilioni ya dola. Baadhi ya watumiaji wa mtandaoni walimsihi mwigizaji huyo angalau amsaidie mtoto wake, ambaye anaishi katika umaskini nchini Kanada.

Uhusiano wa Ng na mamake Elaine Ng Yi-lei uliharibika baada ya kuacha shule na kutoroka na mwenzi wake, Anti, mnamo 2017. Walifunga ndoa huko Canada mnamo 2018.