(+video) Diamond atoboa pua baada ya kutoboa maisha, asutwa kwa kumuiga Harmonize

Hatua hii imewagawanya mashabiki wake baadhi wakisema anaiga Harmonize huku wengine wakisaili kama ni mwanachama wa LGBTQ.

Muhtasari

• Ikumbukwe shoo ya Diamond Malawi inakuja wiki mbili baada ya mshindani wake mkali Harmonize pia kufanya shoo kubwa huko.

Msanii Diamond Platnumz ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kuonekana akitoboa pua kwa ajili ya kuweka kipini.

Msanii huyo wikendi iliyopita alikuwa Malawi, kupiga shoo ambapo alionekana akitobolewa pua.

Ikumbukwe shoo ya Diamond Malawi inakuja wiki mbili baada ya mshindani wake mkali Harmonize pia kufanya shoo kubwa huko, ambayo ilikuwa na mapokezi mema na mafanikio ya kujipiga kifua.

Watu mbali mbali walionekana kutolea maoni mseto kuhusu hatua hiyo ya kutobolewa pua, ambapo baadhi walionekana kumsuta kwa kusema kwamba hiyo ni staili ya wanawake na kumtaja kama shoga kimtindo.

Hii si mara ya kwanza kwa Diamond kuonekana akiwa amevaa pete ya pua. Mnamo 2016, pia alivuma baada ya kushiriki picha yake akiwa amevaa pete ya pua.

Alilazimika kuiondoa baada ya sehemu ya mashabiki wake kwenye Instagram kujibu kwa ukali. Video hiyo inakuja wiki moja baada ya kupata matatizo na wanafamilia yake kutokana na kushindwa kuwatambua watoto wake na Tanasha Donna na Hamisa Mobetto.

Msanii huyo ambaye sasa amejiingiza kweney gumzo pevu la uwezekano wake kuwa mwanachama wa LGBTQ, aliwahi nukuliwa katika mahojiano na DW huko Ujerumani akisema kwamab hayuko tayari kabisa kuingia katika ndoa na mwanadada mwingine baada ya mahusiano yake kadhaa kusambaratika, huku akiwa tayari ana watoto kadhaa na wanawake watatu tofauti – wale wanaojulikana.

Akitetea uamuzi wake, Platnumz alisema kwamba wanawake wanamfanya msanii wa kiume kupoteza dira katika muziki na ndio sababu hataki kujihusisha katika ndoa kwani lengo lake kuu ni kuendelea kuwatumbuiza mashabiki wake kwa vibao moto.