logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akothe asema asipomzalia mpenzi wake mzungu watu wamtukane mbwa

Mwanamuziki huyo alifichua kuwa anataka kuanzisha familia na Schweizer

image
na Radio Jambo

Yanayojiri27 October 2022 - 06:00

Muhtasari


• Akothee aliwapa ruhusa mashabiki wake ya kumsuta akikosa kubeba ujauzito wa Schweizer kwa alivyoonyeshwa mahaba.

Mwanamuziki Akothee alifichua kuwa angetaka kuanzisha familia na mpenzi wake Schweizer kwa jinsi anavyompenda.

Msanii huyo amekuwa akipakia picha zake na mpenzi wake Shweizer katika mitandao ya kijamaii.

Akothee amekuwa akitumia wakati wake na mpenzi wake kufanya shughuli za shambani na nyumbani huku wakionyeshana mahaba.

Alisema ameupenda uhusiano huo na kuwa amejihisi amepata kila kitu alichokuwa anahitaji katika uhusiano wa kimapenzi.

"Huyu nisipomzalia niiteni mbwa," Akothee alisema.

Mashabiki wake walimuunga mkono na kumpongeza kwa kusaidiana na mpenzi wake kufanya kazi ya shambani.

"Huyo usipompa mtoto unarudi Bondo haraka sana," teddy_254_ke alimwambia.

"Ahaa kwa kweli usipomzalia tutakuita mbwa kweli," coastwaterglory alisema.

"Jinsi ulivyokuwa unaketi chini inaonekana tayari ashakupachika mimba," motivations_er aliandika.

"Nashuku una ujauzito tayari, unakaa kuwa na mabadaliko kidogo," ajackim alisema.

Mwanamuziki huyo alisema jinsi alivyopenda kufanya kazi za shambani na mzungu wake.

Alipakia video katika Instastory zake iliyoonyesha akiwa kwenye duka la jumla la kuuza vifaa vya ujenzi na mpenzi wake na kuwashauri mabinti ambao wako kwenye mahusiano kuangazia mambo yatakayowasaidia huko mbeleni wanapojihusisha na wanaume.

Aliwakejeli akina dada ambao hupenda kuwategemea wanaume kuwanunulia vitu ghali visivyokuwa na manufaa makubwa katika maisha yao.

"Dada ukizurura kwenye baa, sisi tunazunguka kwenye maduka ya kuuza vitu vya ujenzi , ukiomba iPhone sisi tunanunua shamba," Akothee aliwaambia.

Mama huyo wa watoto watano alimshukuru Shweizer kwa kumwonyesha mahaba na hata kumletea vifaa vya shambani kutoka Switzerland.

Akothee amekuwa katika uhusiano na mzungu huyo wake kwa muda sasa na alifichua kuwa ako tayari kuwa mke mtulivu.

Alimbandika mpenzi wake jina la majazi la 'Omosh' na hata kumfungulia ukurasa katika mtandao wa kijamii wa Instagram.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved