logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Amber Ray avunja kimya kuhusu madai ya kuvishwa pete ya uchumba na mpenziwe Rapudo

Mwanasoshalaiti huyo alisema kuwa amefurahia hatua hiyo ya mahusiano yao.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri27 October 2022 - 06:46

Muhtasari


• Amber Ray aliwashukuru waliochukua hatua ya kumpongeza hata kabla ya kubaini iwapo ni ukweli alichumbiwa.

•Aliwaambia watu waliodhani kuwa amevishwa pete ya uchumba kuwa bado wakati wa kupiga hatua hiyo haujafika.

Mwanasosholaiti Amber Ray amejibu madai ya kuwa alivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Kennedy Rapudo siku ya Jumatano.

Kupitia Instagram, Amber Ray aliwashukuru waliochukua hatua ya kumpongeza hata kabla ya kubaini iwapo ni ukweli alichumbiwa.

"Nawashukuru nyote kwa jumbe mlizonitumia ila kama kawaida wanablogu wamewachanganya kidogo. Haikuwa sherehe ya kuchumbiwa, ilikuwa ni kuposa tu  (ili wazazi wetu kufahamu kuwa tuko kwenye mahusiano) , hii ilikuwa hatua kubwa sana kwetu," mwanasosholaiti huyo alisema.

Alisema kuwa amefurahia hatua hiyo ya mahusiano yao na kuwa imekuwa jambo bora zaidi kumtendekea maishani.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisherehekea siku hiyo na kuitaja kuwa miongoni mwa siku asizotaka kusahau maishani.

Aliwaambia watu waliodhani kuwa amevishwa pete ya uchumba kuwa bado wakati wa kupiga hatua hiyo haujafika.

"Hebu muache kutuharakisha. Tunachukua hatua za mahusiano yetu siku moja baada ya nyingine na kiukweli napenda kila kitu kinachoendelea. Kennedy Rapudo nimefurahi sana kuwa kwenye safari hii nawe," Amber Ray alisema.

Fununu zilienea kuwa Amber Ray alikuwa amevishwa pete ya uchumba baada ya dadake Ellah Ray kupakia video kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika:

"Hongera dada yangu Amber Ray na Kennedy Rapudo. Mungu abariki muungano wenu. Nimepata kuongeza kaka leo,

Aliwapongeza wapenzi hao kwa hatua hiyo kubwa ila hakufafanua zaidi kama ilikuwa sherehe ya kuchumbiwa ama ya posa. Aidha alimtakia dada yake furaha kwenye mahusiano yake na kutaka waendelee hadi hatua ya ndoa.

"Tabasamu zilizomo kwenye nyuso zenu zisididimie katika jina la Yesu. Mungu awalinde na awatangulie," alisema.

Amber na Rapudo walirudiana wiki tatu zilizopita baada ya kuachana kwa muda.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved