Natamani kupata mtoto wa kiume - Vera Sidika akiri

Sidika alionea wivu uhusiano wa karibu wa bintiye na baba yake Brown Mauzo

Muhtasari

• Vera alisema kuwa  Asia na baba yake wamezoeana sana kiasi cha kukataa kubebwa naye.

Brown Mauzo na Asia

Mwanasosholaiti Vera Sidika amesema kuwa anatamani kuwa na mtoto wa kiume siku za mbeleni ili wawe na ukaribu kama wa bintiye Asia Brown na baba yake Brown Mauzo.

Katika Instastory zake, Sidika alieleza jinsi binti yake ana ukaribu na Brown Mauzo.

Vera alisema kuwa sababu yake ya kutamani kuwa na mtoto wa kiume ni kuwa anauonea wivu urafiki wa karibu ambao Asia na Brown Mauzo wako nao.

"Mpenzi Mungu, naombea maajabu katika maisha yangu, natumai huko mbeleni utanipa mtoto wa kiume . Heh!!Nitamringia mume wangu wacha tu," staa huyo wa 'Popstar' alisema.

Alisema kuwa Asia amekuwa na mazoea ya kushinda na kubebwa kila wakati na baba yake kiasi cha kumkataa yeye.

Mama huyo wa mtoto mmoja alipakia video ya Asia na baba yake wakiwa wamelala baada ya sherehe aliyomfanyia kwa kufikisha mwaka mmoja.

"Asia anapenda kuwa karibu na baba yake sana. Inaumiza lakini hayo ni maisha. Binti yangu huwa hataki nimbebe wakati baba yake yuko karibu au nyumbani. Kiukweli huwa anamlilia baba yake kila wakati ili ambebe," Vera alisema.

Mama huyo wa mtoto mmoja alieleza jinsi binti yake alivyofanana na baba yake kutoka wakati alipojifungua.

Hata hivyo, Vera alifurahia kuwa na mume aliye na uhusiano wa ukaribu na binti yake na kumsaidia kulea mtoto wao.

"Asia huwa hataki kubebwa hata na walezi wake. Wakati ambao anaweza kubali nimbebe ni wakati ambao baba yake hayuko nyumbani lakini tafakari nini? Baba yake huwa nyumbani kila siku na kila wakati," mwanasosholaiti huyo alisema.

Vera alimwandalia bintiye sherehe ya kifahari ya kushereheka siku yake ya kuzaliwa ambapo kila kitu kilikuwa cha kifahari.

Alifichua kuwa nguo ambayo binti yake alikuwa amevaa siku hiyo ilinunuliwa Amerika na ilimgharimu elfu 30.