Vera Sidika Effect: Brown Mauzo na Otile Brown wafananisha mtindo wa nywele

Otile aliwahi chumbiana na Sidika kabla ya Mauzo kumtoa pale na kuzaa na mwanasosholaiti huyo.

Muhtasari

• Wawili hao walitaniwa vikali kwa kuonekana na mtindo sawa wa nywele.

Brown Mauzo, Otile Brown
Brown Mauzo, Otile Brown
Image: Instagram

Wasanii Otile Brown na Brown Mauzo wamezua gumzo kali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana wakiwa wamefananisha mtindo mpya wa kusuka nywele zao.

Brown Mauzo alionekana juzi wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya bintiye na mwanasosholaiti Vera Sidika, Princess Asia Brown akiwa na mtindo mpya wa nywele. Mtindo huo ambao ni wa kusuka nywele fupi aina ya rastas ulikumbatiwa pia na msanii Otile Brown, siku moja tu baada ya kutimba nchini akitokea Marekani alikofanya ziara ya muziki kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Mashabiki na washikadau katika Sanaa ya burudani nchini Kenya hawakusita kuona mfanano huo wa kushabihiana kama shilingi kwa ya pili na hata kuibua utani kwamba mfanano wa mitindo yao ya nywele ni kutokana na kutoka kimapenzi na mwanamke mmoja.

Ikumbukwe kabla ya Mauzo kuchumbiana na Sidika na hata kupata mtoto na yeye ambapo sasa wanaishi pamoja kama wapenzi kwa zaidi ya mwaka mmoja, Vera Sidika alikuwa mchumba wa muda mfupi wa msanii Otile Brown baada ya kuachana katika kile walichafuliana majina mitandaoni kwa njia hasi.

Mashabiki walioona mfanano wa mitindo ya Brown na Mauzo waliwakumbusha sakata hilo na Sidika huku wengine wakitania majina yao ya Brown kuwa sawa pia.

“Tunawaita vijana Brown wa Vera Sidika,” Lucy Calvix alisema.

“Wanafanana kwa njia moja vile walimchumbiana mwakamke mmoja,” mwingine aliibua utani.

“Wanapenda kushare lakini haijalishi, kushare ni kuonesha upendo kwa mwenzako,....mtindo sawa wa nywele, Vera Shikwekwe, na wote ni Browns,” Donelyn Nesh alisema.