"Namtangaza huyu, nampenda!" Diamond adokeza mahusiano na Zuchu

Diamond alitumia alitumia wimbo wa Mbosso 'Huyu Hapa' kukiri mapenzi yake kwa Zuchu.

Muhtasari

• Bosi huyo wa WCB alipakia picha za binti huyo wa Khadija Kopa na kuambatanisha na jumbe zilizodokeza mahusiano kati yao.

•Wawili hao walionekana wakijivinjari kwa mahaba  katika hafla ya uzinduzi wa Mbosso iliyofanyika Alhamisi jioni. 

ZUCHU NA DIAMOND PLATNUMZ
Image: WASAFI/INSTAGRAM

Staa wa Bongo Diamond Platnumz ameendelea kuwachanganya zaidi mashabiki wake kuhusu uhusiano wake halisi na msanii wake Zuchu.

Ijumaa, bosi huyo wa WCB alipakia picha za binti huyo wa Khadija Kopa na kuambatanisha na jumbe zilizodokeza mahusiano kati yao.

Katika picha moja ambayo walipigwa pamoja, Diamond alitumia alitumia wimbo wa Mbosso 'Huyu Hapa' kukiri mapenzi yake kwa Zuchu.

Alichagua neno la wimbo huo,  "Liwalo na liwe, leo namtangaza,sitaki nishauriwe, eh namtangaza, huyu hapa huyu, nampenda," kudokeza kuwa kwa kweli yupo kwenye mahusiano na malkia huyo kutoka Zanzibar.

Katika picha nyingine aliyopakia kwenye Instastori, Diamond alidokeza  kuwa yupo kwenye mahusiano na Zuchu bila kulazimishwa.

"Sijarogwa ndugu yenu, ni mapenzi nayopatiwa, maana kanipa kisavu kipapatilo nyama ya njiwa,huyu hapa huyu, nampenda," alisema kupitia wimbo.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Hata hivyo, hivi majuzi bosi huyo wa WCB alikana madai ya kuwa kwenye mahusiano na Zuchu  na kusema kuwa ni msanii wake tu.

Diamond alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya mmoja wa mameneja wake kumpa shinikizo la kumuoa msanii huyo wake.

Wawili hao walionekana wakijivinjari kwa mahaba  katika hafla ya uzinduzi wa Mbosso iliyofanyika Alhamisi jioni. 

Diamond pia amekuwa akionyesha wivu Zuchu anapowaonyesha watu upendo .

Kwa muda mrefu  sasa Diamond Platnumz na Zuchu wamekuwa wakikisiwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzin ila kufikia sasa mashabiki wao bado hawajaweza kutatua kitendawili cha iwapo wanachumbiana.

Hivi majuzi, Diamond alimbusu Zuchu hadharani baada ya msanii huyo wake kumkabidhi mkufu wa thamani ya kuzaliwa kama zawadi ya siku ya kuzaliwa.