logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwijaku: Harmonize anajua Kuimba si kama Diamond anaiba nyimbo za watu

Hakuta wasanii wanaoandika Tanzania, yaani ukimtoa Alikiba anayefuata ni Harmonize - Mwijaku.

image
na Radio Jambo

Makala01 November 2022 - 08:30

Muhtasari


• Harmonize anajua sana kuandika mashairi yake, tatizo lake moja ni laana. Hakuna mtu aliyetembea na kuku na mayai yake akaishi salama - Mwijaku.

Mwijaku, Diamond Platnumz

Mtangazaji mwenye utata kutoka nchini Tanzania, Mwijaku ameibua madai mengine dhidi ya Diamond huku akimteteac Harmonize kwa ubora wa kutunza mashairi ya muziki.

Mwijaku ambaye alikuwa anazungumza na wanablogu alisema kwamba anatambua fika Harmonzie ana ubora wa kiwango kilochotukuka katika kuandika mashairi ya muziki ila ana tatizo moja la kile alichokiita laana.

Alisema kwamba  msanii huyo kutoka lebo ya Konde Gang ana weledi mkubwa sana lakini pia na kipaji kilichokubuhu katika kuandika vesi nzuri zenye mnato wa aina yake lakini kuna laana inayozidi kumtafuta – ile ya kutembea na Paula ambaye sasa ni binti yake wa kambo.

Alimshauri kwamba kama anataka nyota yake ya kimuziki iendelee kung’aa basi ni sharti aende kwenye matabahu na kutubu dhambi yake ili azidi kukwea kimuziki.

Alisema kwamba Harmonize anakuja wa pili katika wasanii bora wanaoandika mashairi ya kuvutia.

“Hakuta wasanii wanaoandika Tanzania, yaani ukimtoa Alikiba anayefuata ni Harmonize. Anajua sana kuandika mashairi yake, tatizo lake moja ni laana. Hakuna mtu aliyetembea na kuku na mayai yake akaishi salama. Huwezi kutembea na mtoto na mama wote, huwezi kufanya hivo ukafanikiwa,” Mwijaku alisema.

Aliwashauri washikadau katika muziki wanaotaka kuwekeza kweney msanii basi wamchague Harmonize ila kabla ya kuwekeza kwake kwanza wamshauri kumpeleka mskitini kwa ajili ya kutubu.

“Ni msanii ambaye anajua kuimba. Kama unataka kuwekeza wekeza pale ila kwanza mpeleke mskitini. Harmonize anajua sana kuimba, mimi nimezunguka mikoa kadhaa, ana nafasi yake katika jamii, lakini tatizo laana” Mwijaku alishauri.

Pia alimuingilia Diamond na kusema kwamba yeye hana lolote kando kuimba nyimbo za watu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved