Wahu: Mnaoomba nipate mtoto wa kiume, tafadhali elekeza maombi yenu kwingine

Wahu katika siku za hivi karibuni amekuwa akikunjiana mashati na wanamitandao wanaomtia shinikizo la kupata mtoto wa kiume.

Muhtasari

• Mama Shi akiripoti kazini usiku! Wakati huo huo wale wanaoomba nipate mvulana "wakati ujao" tafadhali elekeza maombi yako kwa mtu mwingine - Wahu.

Mabinti wa Nameless; Tumiso, Nyakio na Shiru.
Image: FACEBOOK// NAMELESS

Mwanamuziki Wahu Kagwi ametilia kwenye mizani suala la kushinikizwa na baadhi ya watumizi wa mitandao ya kijamii wanaomtaka kupata mtoto wa kiume baada ya kupata mabinti watatu kwa mfululuzo.

Kupitia chapisho ambalo alilipakia kwenye Facebook yake, Wahu aliwasuta hao wenye mtazamo kuwa anafaa kupata mtoto wa kiume na kusema kwamba hata watuame vipi kwa maombi hawezi wasikiliza.

Aliwataka wenye dhana kama hiyo kuelekeza maombi yao kwingine na wala si kwake kwani hayuko tayati kuingia chini ya shinikizo la kutopata mtoto wa kiume.

“Mama Shi akiripoti kazini usiku! Wakati huo huo wale wanaoomba nipate mvulana "wakati ujao" tafadhali elekeza maombi yako / matakwa yako mema kwa mtu mwingine,” Wahu alisema.

Alizidi kufafanua zaidi akisema kwamba yeye mpaka sasa ameridhika na Baraka ya mabinti watatu ambao tayari ameshabarikiwa nao.

“Mimi kama mimi nimeridhika sana na malaika wangu 3 Mungu amenibariki 🤗💝. Moyo wangu umejaa zaidi 🙏🏾❤️. Vinginevyo usiku mwema Kwa wenye mnalala 🤗😘..” alisema.

Takribani wiki tatu sasa tangu aweke wazi kumpata binti wa tatu, Wahu na mumewe Nameless wamekuwa wakimulikwa na baadhi ya wanamitandao wakiwataka kupata mtoto wa kiume japo mmoja na Wahu hii si mara ya kwanza ameonekana akijibu maswali na matakwa kama hayo.

Wakati mmoja alimjibu mtumizi wa mitandao aliyemuusia kupata mtoto wa kiume ambapo Wahu alisema alisema hana haja kabisa na kupata mtoto wa kiume.

Sina haja ya kumtafuta mtoto wa kiume hata kamwe... Nina furaha na nimeridhika na mabinti wangu," alijibu.