Cebbie Koks awakemea waliotoa maoni machafu kuhusu kifo cha mwanawe Davido

Jumanne kulizagaa taarifa za tanzia kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha mtoto wa msanii huyo.

Muhtasari
  • Mchungaji mmoja kutoka nchini humo aliweka wazi kwamba kifo cha mtoto wa msanii huyo ni moja ya mambo ambayo aliyatabiri mapema mwaka huu
Cebbie Koks
Image: Hisani

Dada yake msanii maarufu nchini Akothee,Cebbie Koks kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewakamea wanamitandao ambao walitoa maoni machafu kuhusu kifo cha mwanawe msanii wa Nigeria Davido.

Jumanne kulizagaa taarifa za tanzia kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha mtoto wa msanii huyo.

Huku baadhi yao wakituma jumbe za rambirambi,kuna wale ambao hawakuwa na utu wa moyo kwani walizungumza mabaya yote kuhusu kifo cha mtoto huyo.

Baada ya maoni yao machafu Cebbie hakuridhishwa kabisa, kwani aliwashauri wanamitandao sio kila kitu au jambo la kutolea maoni mitandaoni.

Cebbie aliweka wazi kwamba hakuridhishwa na baadhi ya maoni hayo.

"Sio lazima utoe maoni kwa kila kitu hata kama unahisi unapaswa kutoa maoni,nimehuzunika kwa ajili ya maoni kuhusu kifo cha mwanawe msanii Davido na mkewe Chioma 

Kujithibiti ni kujua kitu na kuwa na haki ya kukizungumzia kisha unakataa kukizungumzia,"Cebbie Alisema.

Mchungaji mmoja kutoka nchini humo aliweka wazi kwamba kifo cha mtoto wa msanii huyo ni moja ya mambo ambayo aliyatabiri mapema mwaka huu.

Kulingana na mchungaji huyo kwa jina nabii Samwel King, mnamo Januari tarehe 7 mwaka huu alitabiri kifo cha mtoto wa msanii Davido ila akapuuziliwa mbali alipotaka kukutana na familia yake ili kuwataarifu kuhusu utabiri huo.

Alisema kwamba huo ni mwanzo tu kwani atazidi kutoa ufunuo zaidi kuhusu utabiri huo alioutaja kama uliotimia na kuonya watu dhidi ya kupuuza utabiri unaotokana na manabii wa Mungu.