Eric Omondi agharamika zaidi ya laki 2 kwa mavazi ya sherehe ya Amber Ray

Omondi alilalamika baada ya sherehe ya kuzaliwa ya Amber Ray kughairiwa

Muhtasari

• Omondi alisema aligharamika zaidi ya laki mbili kununua nguo zake na mpenzi wake kwa ajili ya sherehe hiyo iliyokuwa na mtindo maalum wa kuvaa.

• Mchekeshaji huyo alilalamika baada ya sherehe hiyo kughairiwa.

Eric Omondi na mpenzi wake Lynne
Image: ERIC OMONDI//INSTAGRAM

Mchekeshaji Eric Omondi amelalamika baada ya mwanasosholaiti Amber Ray kughairi mipango ya shrerehe yake ya kuzaliwa.

Kwenye Instagram, Omondi alitangaza kuwa alikuwa ashafanya mipango ya kujitayarisha kwa ajili ya sherehe hiyo.

Alisema kwamba alikuwa ametumia pesa nyingi kununua nguo zake na za mpenzi wake ili kuhudhuria sherehe hiyo.

"@iam_amberay umetukosea sanaa yaani mpaka tuliagiza kutoka ng'ambo nguo zinazofanana za rangi ya  Pastel Pink.  Nguo ya @l.y.nn.e iligharimu zaidi ya shilingi laki 1 na yangu shilingi elfu 97 .Hiyo 210,000 afadhali ningekupa. Hata hivyo, Heri njema ya kuzaliwa...@kennedyrapudo MKO?" Omondi alisema na huku akipakia video yake na mpenzi wake wakionyesha nguo walizokuwa wamenunua kwa ajili ya sherehe hiyo.

Hii ni baada ya Amber kuwaalika baadhi ya watu maarufu kwa sherehe hiyo ya kibinafsi na kuwapa mtindo wa kipekee wa mavazi kwa hafla yake.

Baadaye Amber alifutilia hafla ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa na kuwaambia watu kuwa mpenzi wake alikuwa na mipango mbadala.

"@ericomondi @l.y.nn.e Weh! Afadhali hivyo nilighairi juu hakuna vile mngeng'ara kunishinda 🙆🏻‍♀️🙌🏼 ….. poleni Aki…..mapenzi ya Kijaluo yameniweza🤭," Amber alimjibu Omondi.

Siku ya kuzaliwa ya mwanasosholaiti huyo ni leo Ijumaa Novemba terehe 4,  lakini mpenzi wake Rapudo aliamua kumuandalia hafla ya kufana siku ya Alhamisi siku moja kabla ya Ijumaa.

Rapudo alimwandalia Amber sherehe ya kipekee ambayo walikunywa mvinyo na kula keki kisha kumzawadi simu ya kifahari ya iPhone 14 Pro Max.

Amber Ray anafikisha miaka 31 leo Ijumaa.