logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mapenzi na Kazi: Wachumba ambao pia ni washirika kikazi

Hawa ni wale waliokiuka dhana ya kuwa mapnezi kazini hayawezi yakapaliliwa na kua.

image
na Radio Jambo

Habari04 November 2022 - 05:29

Muhtasari


• Hapa tunakuandalia orodha ya baadhi ya Wakenya maarufu ambao wamefanikiwa pakubwa kukiuka dhana hizo zinazoonya dhidi ya kuwa na mpenzi ambaye mnafanya kazi pamoja.

Wachumba wanaofanya kazi pamoja

Kuna dhana nyingi tu zinazohusisha mapenzi na kazi, wengi huonya dhidi ya kujiingiza mapenzi na mtu ambaye mnafanya kazi pamoja, lakini je, unafahamu wapo baadhi ya Wakenya maarufu ambao ni wachumba au wapenzi na wanafanya kazi kwa pamoja?

Hapa tunakuandalia orodha ya baadhi ya Wakenya maarufu ambao wamefanikiwa pakubwa kukiuka dhana hizo zinazoonya dhidi ya kuwa na mpenzi ambaye mnafanya kazi pamoja.

Wahu na Nameless

Hao ni wapenzi wa zaidi ya miaka 25 ambao wanasherehekewa sana kuwa watu maarufu waliokiuka dhana zote zinazolenga kutoa tafsiri kuwa mapenzi na kanzi haviwezi vikaendana. Katika safari yao ya pamoja kama wapenzi kwa miaka 25 iliyopita, Wahu na Nameless wanajivunia ndoa imara na mabinti watatu juu.

Wamekuwa wakishirikiana katika kazi za kimuziki miaka hiyo yote na mwaka jana waliachia collabo yao ya Back It Up ambayo mpaka sasa inazidi kufanya vizuri katika masoko mbalimbali ya kidijitali ya kupakua miziki.

Lulu Hassan na Rashid Abdalla

Watangazaji mashuhuri wa habari ambao hutumika kama mfano bora kwa wengi kwenye mitandao ya kijamii. Lulu na Rashid wanafanya kazi pamoja kwenye Citizen TV kama waandaaji wenza wa taarifa ya habari ya Nipashe ya Citizen.

Diana Marua na Bahati Kioko

Wapenzi hawa wawili ambao wiki hii walimpokea mtoto wao Malaika wamekuwa wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu tangu msanii Bahati aache kuwasajili wasanii wapya kwenye lebo ya EMB.

Pamoja kama wachumba, wamekuwa wakishirikiana katika miradi mbali mbali ya nyimbo huku wakitoa collabo zilizoteka anga na kupendwa na wengi.

Milly na Kabby wa Jesus

Hii ni familia ya wanablogu wa mtandao wa YouTube ambao wamefanikiwa kufanya kazi pamoja na kupata ufanisi usiomithilika kutokana na ushirikiano wao wa kuunda maudhui ya YouTube.

Wameonyesha mtindo wa maisha unaoongozwa na kudumishwa na mikataba ya ubalozi wanayopata kutoka kwa makampuni mbali mbali kutokana na ufuasi mkubwa walionao kwenye chaneli yao ya pamoja ya YouTube.

Milly Chebby na Terence Creative

Terence Creative na mkewe Milly Chebby

Milly Chebby na Terrence Creative hutengeneza video pamoja, wakionyesha taratibu zao za maisha ya kila siku na mambo mengine yanayozunguka maisha ya kila siku ambayo huburudisha wafuasi wao. Hukuwakiwa wamedumu pamoja kwa zaidi ya miaka 10, wawili hawa wamefanikiwa pakubwa kutokana na mitikasi yao ya mitandaoni.

Mungai Eve na Trevor

instagram KWA HISANI

Moja kati ya wanandoa mashuhuri wachanga zaidi nchini Kenya. Mungai Eve na mpenzi wake ambaye pia anajiongeza kama muongozaji wa video zao walianza kutoka chini hadi sasa wanatamba katika tasnia ya burudani kwani wana chaneli ya YouTube inayokua kwa kasi pamoja ambayo ni biashara yao yenye malipo kama wanandoa.

Celestine na Njugush

Njugush na Celestine wamefanikiwa sana kwenye YouTube wakitengeneza skits za kuchekesha ambazo zimewafanya waendelee kuunda maudhui zaidi pamoja kwenye mitandao ya kijamii.

Pamoja wamefanikiwa kununua nyumba nzuri na wana watoto wawili, mwa pili wakitangaza kumkaribisha hivi majuzi. Wamekuwa wakifanya mwendelezo wa filamu yao ya Through Thick &Thin ambayo inasimulia jinsi waligandiana tangu wakiwa bila kitu mpaka sasa wakiwa angalau na utajiri wa kusitiri maisha yao ya kila siku.

Kate Actress na Phillip Karanja

Phil na Kate Actress walipata upendo kwa kila mmoja wakati wakifanya kazi pamoja. Kate, ambaye jina lake halisi ni Catherine Kamau, aliwahi kusimulia hadithi ya jinsi yeye na mumewe walipatana. Alisema awali hawakuweza kusimama kila mmoja kwenye seti. Hivi sasa, wanandoa wana kampuni yao ya uzalishaji kwa jina la Phil It Productions.

 

 

Judy Nyawira na Abel Mutua

katika hafla ya awali.

Abel Mutua amekuwa akimtumia mkewe Judy Nyawira kama mtayarishaji/meneja wake. Judy hupanga matoleo mengi ya Abel kwenye YouTube, kazi ambayo mashabiki wao wengi wamewasifia.

Nadia Mukami na Arrow Bwoy

Wawili hao ambao miezi michache iliyopita walimkaribisha mtoto wao wa kwanza wamekuwa wakifanya muziki pamoja kabla na hata baada ya kupendana.

Nadia Mukami na Arrow Bwoy walishirikiana katika nyimbo kadhaa na wimbo wao wa hivi majuzi, 'Kai Wangu' uliochochewa na mtoto wao wa kiume.

Jackie Matubia na Blessing Lungaho

Kuna habari kwamba waigizaji hao mahiri walikutana kwenye seti ya kipindi cha Zora wakati Jackie Matubia akicheza 'Nana' na Blessings akacheza 'Madiba'.

Wawili hao walioigiza 'struggle love' hivi majuzi walimkaribisha mtoto wao wa kwanza pamoja na pia wamechumbiana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved