Diana Marua asherehekea siku ya kuzaliwa kwa picha nusu uchi, apokezwa matusi

Mashabiki walidai kuwa mpiga picha wa Diana alikuwa anapata wakati mgumu kumpiga picha.

Muhtasari

• Hata hivyo, mashabiki wake hawakufurahishwa na mama huyo kupakia picha zake akiwa nusu uchi na kumzomea.

Image: Instagram

Rapa Diana Bahati amegeuka gumzo Instagram baada ya kupakia picha akiwa nusu uchi katika ukurasa wake wa Instagram.

Diana aliapakia picha hiyo huku akijitakia heri njema ya kuzaliwa akiwa hospitalini, keshajifungua mtoto wake wa tatu.

“Heri ya kuzaliwa kwa mama wa hivi karibuni mjini,”Marua aliandika.

Hata hivyo, mashabiki wake hawakufurahishwa na mama huyo kupakia picha zake akiwa nusu uchi na kumzomea.

“Kufichua uchi wako ili kuwa kutafuta kiki,”jayvashmateo aliandika.

“Una mandugu, fikiria hilo kabla ya kufanya hili,”jeremykebee alsema

Mashabiki pia walishangazwa na msanii Bahati kuwa sawa na jambo ilo alipomtakia mema mke wake katika chapisho hilo.

“Mama Malaika Bahati, umeamuaje?  Heri ya kuzaliwa malkia wangu,” Bahati alisema.

Baadhi ya maoni ya wanamitandao baada ya Bahati kutoa maoni yake ni:

“Sasa kusema ukweli anaonyeshana mwili wake na uko sawa na hilo?”faizasalim983 aliandika.

“Ambia mke wako aache kufichua uchi wake kwa sana,” dream_girl_ke alisema.

“Heri ya kuzaliwa Dee, Mungu akubariki na nguo ili uweze kusitiri mwili wako,”violet.violah.587 alisema.

“Kwa kweli umeanguka mtihani wa kuwa mwanaume wa nyumba. Unafaa kuwa na mabidiliko au utapotea,” thee_malvinas_show alisema.

Hii si mara ya kwanza mama huyo wa watoto watatu kupakia picha akiwa nusu uchi mtandaoni ila wakati huo mwingine alikuwa amejisitiri kidogo.

Mashabiki wake hawakumsuta wakati huo ila baadhi yao walizungumzia suala la mpiga picha wake kuwa na wakati mgumu akimpiga picha kwa kuwa nusu uchi.