logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize awashambulia Zuchu na Diamond akimpa kwaheri Anjella, "Sikuwahi kumshika makalio"

Nilimheshimu Anjella kama dadangu ambapo sikuwahi kumshika makalio kama wanaume wengine - Harmonize.

image
na Radio Jambo

Burudani05 November 2022 - 10:26

Muhtasari


• Alisema kuwa amesikitishwa na chawa wote wanaomsema kuwa kamdhulumu Zuchu hali ya kuwa hawakuwahi kufungua mdomo kipindi anamsapoti.

Harmonize amshambulia Diamond kwa kumshika Zuchu Makalio

Msanii Harmonize anaonekana kutomaliza ugomvi wake na aliyekuwa baba yake kimuziki Diamond Platnumz hivi karibuni.

Harmonize katika kila jambo ambalo amekuwa akilifanya amekuwa akimrushia Diamond vijembe kutoka pande zote.

Jumamosi alikuwa anamuaga Anjella kutoka lebo ya Konde Music Worldwide ambapo aitumia nafasi hiyo kuelezea uhusinao wake na Anjella kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita tangu kumpa mkataba kama msanii wake.

Harmonize alisema kwamba yeye amekuwa akimheshimu Anjella na wala hakuwahi kumshika makalio na kumbusu kama wanavyofanya wasanii wengine, hapa akionekana kumrushia dongo Diamond na Zuchu ambao kwa muda sasa wamekuwa wakisemekana kuwa katika mapenzi ya siri.

Alionesha kusikitishwa kwake na uvumi unaondelezwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu sakata la kuondoka kwa Anjella huku akidokeza kuwa machawa wamelipwa ili kulipaka jina lake tope kuwa anamdai Anjella mamilioni kadhaa kabla ya kumkubalia kuondoka na kazi zake za kimuziki pamoja na kurasa za mitandao ya kijamii.

“Nipo hata natazama kwa hamaki jinsi watu wanazungumza utumbo kuhusu mimi na dadangu Anjella. Kwa kweli huwa sifuatilii sana, lakini inachekesha kwamba wakati ambapo nilimshika mkono kumpa sapoti, kumheshimu kama dadangu ambapo sikuwahi kumshika makalio kama wanaume wengine wanaowapa visenti vya kula, hakuna aliyefungua mdomo. Leo chawa wote fyookoo fyookooo fyoookooo,” Harmonize alishambulia.

Kuondoka kwa Anjella kwenye lebo ya Konde Gang kunatokea mwezi mmoja tu tangu wasanii Killy na Cheed kuondoka pia katika lebo hiyo mnamo Oktoba 10.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved