"Nikifa na kuna jamaa anakufinyia jicho, songa naye" - Mutua amshauri mkewe Judy

Mkurugenzi kama anavyojiita alisema hilo ni jambo ambalo wamelizungumzia na mkewe kwa muda mrefu tu na kuwa na maelewano.

Muhtasari

• Kama kuna janaa huko anakufinyia macho, aai kwani ni kesho, dakia hiyo fursa,” Abel Mutua alizungumza - Mutua.

Abel Mutua na mkewe
Abel Mutua na mkewe
Image: Instagram//AbelMutua

Muhongozaji wa filamu Abel Mutua amezungumza ukakasi uluoko kwenye ukweli wa maneno ambayo huwa anamwambia mkewe Judy Nyawira kufanya endapo atatangulia mbele za haki.

Abel na Judy walikuwa wanazungumza kwenye podcast ya The Joy Ride kwenye YouTube ambapo walizungumzia mambo mengi kuhus vile walipatana na mpaka sasa hivi jinsi maisha yao ya ndoa yanavyoenda.

Abel alisema kuwa anampenda mkewe kwa kumvumilia katika mambo mengi ya kuudhi ambayo yeye huyafanya huku Nyawira akisema kwamba anamkubali sana Abel kutokana na heshima anayomuonesha kila muda.

Abel alirushiwa swali la iwapo anamusia mkewe kuolewa na mtu mwingine endapo atafariki, alijibu kuwa ni kitu ambacho huwa anamuambia kila mara kuwa ikitokea ametangulia mbele ya haki basi asibaki akiteseka kimawazo kwani ana uhuru wa kuchumbiana na mtu mwingine.

Ni kitu tushawahi kuzungumzia mara kadhaa nikamwambia kuwa tafadhali songa mbele na maisha juu usikae hapo ukiomboleza na mimi nishamalizxa kazi yangu duniani, tafakari tu na uendelee na maisha na mtu mwingine. Kama kuna janaa huko anakufinyia macho, aai kwani ni kesho, dakia hiyo fursa,” Abel Mutua alizungumza kwa vichekesho.

Hata hivyo, wawili hao walisema kuwa wlikutana mara ya kwanza mwaka 2008 na walikuwa wanapata pesa vizuri sana ila matumizi kidogo yalikuwa yanawashinda kutokana na ubadhilifu waliokuwa nao.

Mutua na mkewe walisema kwamba iliwachukua muda mpaka hivi majuzi 2020 ndio walipata elimu kidogo kuhusu jinsi ya kuendesha pesa ndio wakawa watu wa kuwajibikia kila senti wanayoipata.